Pre GE2025 Mwenyekiti UVCCM Mara awataka vijana kusaidia kuzuia wizi wa mifugo Rorya

Pre GE2025 Mwenyekiti UVCCM Mara awataka vijana kusaidia kuzuia wizi wa mifugo Rorya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Kufuatia matukio ya mara kwa mara ya Wizi wa Mifugo katika Wilaya ya Rorya, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama cha Mapinduzi Mkoani Mara, Mary Daniel amewataka Vijana wilayani Rorya kuacha kuvinyoshea vidole vyombo vya Dola kukomesha Vitendo hivyo badala yake na wao kuwa mstari wa mbele kuwaweka wazi wanaoshiriki katika matukio hayo.

1741771677040.jpeg

Mary ametoa kauli hiyo Wakati akizungumza na Vijana na makundi mbalimbali wakiwemo bodaboda, Mama Ntilie pamoja na Wavuvi ambapo amesema ili kuhakikisha vitendo hivyo vinakoma, Vijana wana wajibu wakuvisaidia vyombo vya Usalama katika mapambano hayo.

Soma, Pia: Mwenyekiti UVCCM Geita: Hatufurahishwi kuona vijana wetu wanaondoka duniani kwa kutekwa! Tunalaani na kukemea matendo haya!

"Usitegemee hivi vitendo vinafanyika nyinyi hamjui au Wanaofanya hatuwajui tunatakiwa kuwataja, wahusika tunawajua lakini pia muweke ulinzi shirikishi hatutarajii kusikia na nyinyi mnalalamika" - Alisema Mary Daniel Mwenyekiti wa UVCCM Mara.

1741771771465.jpeg
Baadhi ya vijana wamesema si kwamba hawashiriki katika kukabiliana na matukio hayo ya Wizi, lakini wamekuwa wakiwakamata wezi na wanapowafikisha kwenye vyombo vya Dola, wanaachiwa huru.

1741771733829.jpeg
 
Kazi ya vyombo vya ulinzi ni hipi.
Sawa na huku mikoani unalipishwa pesa ya usafi madukani alafu wanataka ufanye usafi wewe .wao waje kuchukua takataka.
 
Back
Top Bottom