Mwenyekiti UVCCM Mkoa akamatwa kwa tuhuma za wizi!!NA huyu nae

Mwenyekiti UVCCM Mkoa akamatwa kwa tuhuma za wizi!!NA huyu nae

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Mwenyekiti UVCCM Mkoa akamatwa kwa tuhuma za wizi
Joyce Joliga, Songea

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Mkoa wa Ruvuma, Benedict Ngwenya, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za wizi wa Sh 76,500,250.00, mali ya Kampuni ya Dan and Associates Enterprises Ltd, iliyoko wilayani Mbinga.


Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma, Michael Kamuhanda alisema, Ngwenya ni mwajiriwa wa kampuni hiyo inayonunua na kukoboa kahawa mwenye cheo cha Meneja mwangalizi wa mitambo ya kukoboa kahawa.


Alisema, Ngwenya kwa nyakati tofauti, kati ya Novemba 12 mwaka juzi, na Agosti 19 mwaka jana, alichukua fedha kutoka Makao Makuu ya kampuni kwenda kwenye mitambo iliyoko vijijini, akidai anapeleka kuwalipa wafanyakazi, pamoja na kununua baadhi ya vifaa kwenye mitambo hiyo, lakini imegundulika kuwa fedha hizo hazikufika kwa walengwa.


Alisema baada ya Kampuni kugundua udanganyifu huo, ilifanya ukaguzi na kugundua kwamba fedha hizo ziliibwa, ndipo ilipoamua kuripoti kituo kikuu cha polisi cha Mbinga.


Kamanda alisema Kampuni hiyo, ina mitambo 16 ya kukoboa kahawa ambayo ipo katika vijiji vya Litembo, Linda, Mihindo, Mikaranga, Ukuli na Nyoni Makolo.


Alivitaja vijiji vingine venye mitambo hiyo kuwa ni Lugali, Kihangi Mahuka, Mahilo, Nsasa, Ulwambo, Matekela, Ngima, Minungu, Kitumbi na Uluwa.


"Uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa, Ngwenya akiwa msimamizi mkuu wa mitambo hiyo, Desemba mwaka jana aliingia kwenye kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Ruvuma, ambapo alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, jambo ambalo linaleta picha kuwa fedha hizo huenda zilitumika kwenye shughuli za kampeni ya uchaguzi," alisema.


Kamanda alisema polisi wanaendelea kufanya upelelezi wa kina, na kwamba utakapokamilika, Ngwenya atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya wizi wa fedha za mwajiri wake.
 
Back
Top Bottom