Pre GE2025 Mwenyekiti UVCCM Mwanza: Vijana hakikisheni CCM inaendelea kushika Dola

Pre GE2025 Mwenyekiti UVCCM Mwanza: Vijana hakikisheni CCM inaendelea kushika Dola

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Ndio nilichokuwa nasema, CCM hata chawa anapewa anafundishishwa ili kwenye urpokaji wake akafanye kazi iliyotukuka jambo ambalo kwa upinzani wakosa, mwisho wa siku wanaishia kwenda ovyo ovyo kila mtu anatoa tamko kama mahindi ya bisi,

====



Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mwanza, Ndg. Seth Benard Masalu, amewapongeza vijana wa CCM kwa ushindi mkubwa wa zaidi ya asilimia 90 katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 27 Novemba 2024.

Akizungumza katika hitimisho la mafunzo ya Viongozi Vijana wa CCM yaliyofanyika wilayani Nyamagana, Masalu alisisitiza umuhimu wa maandalizi kabambe kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Masalu aliwataka vijana wa CCM kutumia maarifa waliyopata katika mafunzo hayo kama silaha ya kuhakikisha ushindi wa chama unaendelea. “Huu sio muda wa kulegea, ni wakati wa kupambana kwa nguvu zote kuhakikisha CCM inashika dola tena na kuleta maendeleo endelevu,” alisema kwa msisitizo.

“Vijana, tusiwape nafasi wapinzani! Ni wakati wa kujitoa kwa hali na mali. CCM ni nguzo ya maendeleo, na ushindi wetu ni ushindi wa taifa,” alihitimisha.
 
Back
Top Bottom