Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Lengi la kauli kama hii ni kumlenga nani? Kuna wanasiasa hapa Tanzaniq familia zako ziko nje ya nchi.
Naomba kujuzwa
======================
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Songwe, Fatma Hussein, anasema anakerwa na baadhi ya wanasiasa ambao wanaifanya Tanzania kama 'gheto' na siyo makazi rasmi kutokana na familia zao kuishi nje ya nchi.
Fatma ameyasema hayo Februari Mosi, 2025 alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari mjini Songwe, kwa lengo la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha mkutano ulimalizika hivi karibuni wa Nishati Afrika.
Amesema wanasiasa hao ndio vinara wa kuchochea na kutoa lugha zinazolenga kudhoofisha utulivu wa nchi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Mtu asiye kuwa na familia hapa nchini anajua hata akivuruga mambo, yeye familia yake ipo salama na kesho ataka tiketi anaondoka, ndio maana nasema lazima Watanzania tuwe makini na hawa watu," amesisitiza Fatma.