Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dodoma, Abdulhabib Mwanyemba, amesema endapo Uchaguzi Mkuu hautafanyika kama ilivyopangwa, serikali iliyopo madarakani inaweza kukosa kutambuliwa kitaifa na kimataifa.
Mwanyemba ametoa kauli hiyo wakati wa Mkutano Maalum wa Mabinti wa UVCCM wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), uliolenga kuwaelimisha vijana juu ya misingi ya CCM na kuwahamasisha kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu ujao.
“Sisi vijana wa CCM tunatakiwa kutoa elimu kwa vijana wenzetu kwamba tunapaswa kushiriki uchaguzi. Hatutakubali kuona Katiba ya Tanzania ikikanyagwa na vikundi vya watu wachache