Mwenyekiti UWT Dar, Mwajabu: Juhudi zetu wanawake hazipotei bure zimepelekea kuinuana kiuchumi

Mwenyekiti UWT Dar, Mwajabu: Juhudi zetu wanawake hazipotei bure zimepelekea kuinuana kiuchumi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

JUHUDI ZETU WANAWAKE HAZIPOTEI BURE ZIMEPELEKEA KUINUANA KIUCHUMI NA NDIO DHAMIRA YA RAIS DKT. SAMIA - CDE. MWAJABU

Ahimiza Wanawake kuendelea kuelimisha jamii juu ya usawa wa kijinsia na kupinga ukatili haswa kwa watoto.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) Mkoa wa Dar es salaam Ndugu. Mwajabu Mbwambo, ameshiriki katika hafla ya Usiku wa Mwanamke wa Kigamboni akiwa ndiye Mgeni rasmi katika hafla hiyo ikiwa ni katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika tarehe 8 Machi, 2024.

WhatsApp Image 2024-03-07 at 10.32.00.jpeg

Katika hotuba yake, Cde. Mwajabu ametanguliza shukrani kwa uongozi wa halmashauri ya manispaa ya Kigamboni kwa kumteua kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo kwani ni heshima kubwa kwake.

Cde. Mwajabu ametoa wito kwa Wanawake wote kwa kuwa na moyo wa kushikana mikono, kuinuana na kupeana fulsa mbalimbali katika kupelekea kuinuka kwenye uchum wa kati.

WhatsApp Image 2024-03-07 at 10.31.35.jpeg

"Nitoe pongezi kwetu sote wanawake kwani juhudi zote tunazofanya wanawake hazipotei bure kwakuwa kwa pamoja tunainuana na ndio dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan."

"Kupitia Serikali, Taaisisi na Mashirika binafsi, Wanawake tumekuwa tukiwezeshwa katika kuingia kwenye uchumi wa kati na kupelekea kuwa chachu ya maendeleo kuanzia kwenye familia hadi jamii kwa ujumla na hali hii imeakisi moja kwa moja kwenye kauli mbiu yetu"

WhatsApp Image 2024-03-07 at 10.32.00(1).jpeg

"Wanawake tuendelee kuelimisha jamii juu ya usawa wa kijinsia na kupinga ukatili haswa kwa watoto na hii ianzie majumbani kwetu katika kutoa Elimu kwa watoto namna ya kuweza kujiepusha na majanga haya."

Ndugu. Mwajabu Mbwambo
Mweyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es salaam.

📍Barakuda Hall - Mjimwema
🗓️ 6 Machi, 2024

#UsikuWaWanawakeKigamboni
#KigamboniMpya
#KaziIendelee
 
Back
Top Bottom