Mheshimiwa JK mimi naamini wewe ni Kiongozi mwenye uwezo mkubwa,na naamini kuwa uko katika grade ya viongozi wenye hekima na busara.
Katika suala la usuluhishi wa mgogoro wa Kenya inakulazimu kushughulikia suala la mgawanyo wa madaraka,bila kusahau kutilia maanani la jinsi uchaguzi ulivyokuwa na dosari zake, na hiki ndicho kiini cha matatizo yote.
Huko kuna utakabiliana na watu wasiotaka kuleta maridhiano kwa kuwa katiba iliyopo inawafanya miungu wadogo.Hawa ni wale wanaomzunguka Kibaki na kumpa ushauri wa kutoleheza kamba.Hwa hawaoni madhara yaliyojitokeza na wala hawaangalii huko mbele kutatokea nini.Staili yao ni kama ile ya Charles Taylor na wenzake,Mobutu Seseseko,Robert Mugabe na wengineo.
Ugumu wa kupata suluhu uko hapo kwa kina Martha Karua,Michuki,Njenga Karume na wengineo.Kama utaweza kumkabili Mzee Kibaki na kumwambia kuwa huko mbele kuna hatari ya kupelekwa kwenye Mahakama ya Kimataifa kwa kuibomoa amani ya Kenya ili kufuata kundi la Michuki na wenzake,ambao walimlazimisha Kivuitu kutangaza matokeo batili,pengine Mzee kwa kuwa ni Mkristo mzuri anaweza kujirudi na kuamua ku save face kwa kukubali na kuridhia hoja ya ODM.
Ujasiri wa kutangaza matokeo ya uwongo ambayo yalisababisha vifo vya watu wengi na kuwaacha wengine wakiwa wakimbizi katika nchi yao ni dhambi isiyosameheka na yote hii itakuwa ni Kibaki na wale wapambe wake.
Sasa iwapo wale waliopora kura watakubali maridhiano basi kuna bima dhidi ya wao kufikishwa kwenye mahakama ya haki za binadamu huko the Hague na watakuwa wamesalimisha nafsi zao.Vinginevyo historia itakuja kuwahukumu kama ilivyofanya kwa viongozi wengi wa aina hii.
Nakutakia kila la kheri JK.
Hao wengine wanaokubeza kuwa hujui Kiingereza wna chuki tu na katika kila nchi wapo.Dawa yao ni kuwapuuza.Kiingereza ndiyo nini??Si ni lugha tu.