LGE2024 Mwenyekiti wa BAVICHA Dodoma afichua madhaifu na ubadhirifu unaoendelea kwenye zoezi la uandikishaji wa wananchi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

LGE2024 Mwenyekiti wa BAVICHA Dodoma afichua madhaifu na ubadhirifu unaoendelea kwenye zoezi la uandikishaji wa wananchi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Aisha Madoga, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) Mkoa wa Dodoma, amekosoa uandikishaji wa wananchi katika Daftari la Mkazi katika baadhi ya vituo, akisema si sahihi kuwaandikisha wananchi bila kuwapa taarifa kuhusu namba zao.

Aliyasema hayo alipofika kujiandikisha katika Kituo cha Site 1, Jijini Dodoma, katika mchakato unaoendelea kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, mwaka huu.

Soma pia: Godbless Lema: Nendeni mkajiandikishe ili wakishinda kwa wizi, tujue wameshinda kwa wizi!

Madoga alieleza kwamba alikumbana na changamoto ya majina kuandikishwa bila kupewa namba za 'serial', jambo ambalo alidai linaweza kuwa na kusudi baya.

Pia, aliongeza kuwa wananchi wengi hawana uelewa wa kutosha kuhusu mchakato wa uandikishaji, kwani zoezi hilo linachanganywa na uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, hali ambayo inachanganya umma.


Source: Jambo TV
 
Back
Top Bottom