johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
MWENYEKITI wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (BAVICHA), John Pambalu ameeleza kuwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara Tundu Lissu katika kupiga vita fedha chafu zinazotajwa kuzunguka ndani ya chama hicho.
Pambalu alitoa kauli hiyo juzi jijini Mwanza na kueleza kuwa kuendelea kutumika na kuzunguka kwa fedha hizo kunaweza kudhohofisha chama hicho hususani katika kipindi hiki cha uchaguzi wa ndani.
Alidai kuwa kwa kipindi cha nyuma walizoea kushuhudia wanachama wao wakinunuluwa na kuhamishiwa vyama vingine lengo likiwa ni kukimaliza nguvu Chadema na kudai kwa sasa utaratibu umebadilika kwani baadhi ya wanachama wananunuliwa na kubakishwa ndani ya chama ili wakivuruge zaidi.
"Mimi kama Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, ninapinga matumizi ya fedha kwa maana ya rushwa, chama chetu hakikufika hapa kwa vipande vya fedha vinavyotilewa wakati wa uchaguzi,"
"Kama wajumbe watachagua kwa kushawishiwa na vipande vya fedha waelewe wanachama wetu walikimbie vya vingine na kuja Chadema kwa kukimbia rushwa hawatokaa nasi tena kwahiyo niseme tu ukweli mimi napinga rushwa,"alisisitiza.
Alitaja viashiria vya matumizi ya rushwa katika uchaguzi wa ndani ngazi ya kanda kuwa ni pamoja na kusafiri wajumbe,kuwalipa posho pamoja na kuwalaza hivyo kuzionya kanda zote zinazoendelea na uchaguzi kuwa makini na vitendo hivyo na kuacha mara moja kwani havina afya kwenye Chama.
Aidha aliwataka vijana kutumia fursa na nguvu zao ipasavyo katika kushiriki kikamilifu katika uchaguzi unaoendelea ndani ya chama na kujiandaa pia kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na uchunguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika 2025.
Katikati mwa mwezi Mei, mwaka huu Chadema kilitoa baraka kwa baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali za Kanda ndani ya chama hicho kuanza kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa wajumbe wao ili kuwapitisha na kungoza kanda nne za kiutawala ambazo zipo katika mchuano huo.
Waliopitishwa na Kamati Kuu kugombea nafasi ya Mwenyekiti kwa Kanda ya Victoria ni Hezekiah Wenje ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Nyamagana na John Pambalu, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chama hicho (BAVICHA).
Kanda ya Nyasa ni Joseph Mbilinyi (Sugu) na Peter Msigwa, Kanda ya Magharibi ni Dickson Matata, Gaston Garubindi, Mussa Mafure na Ngassa Mboje huku Kanda ya Serengeti akiwa ni Gimbi Massaba na Lucas Ngoto.
Kwa mujibu wa Katibu wa Chadema Kanda ya Victoria Zacharia Obad uchaguzi huo inatarajiwa kufanyika Mei, 25 mwaka huu katika Manispaa ya Bukoba.
Source: Nipashe Digital
My take: Tunywe mtori nyama tutazikuta chini.