Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi: Miradi isiyozidi Bilioni 50 wapewe makandarasi wazawa

Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi: Miradi isiyozidi Bilioni 50 wapewe makandarasi wazawa

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) Mhandisi Joseph Nyamhanga, amezitaka Taasisi za Umma kuzingatia sheria ya ununuzi wa umma ya mwaka 2023 na kanuni zake za mwaka 2024 ambazo zinaelekeza kuwa mikataba ya miradi ambayo haizidi Shilingi bilion 50 inatakiwa itekelezwe na makandarasi wazawa.

Amesema hayo tarehe 20 Februari, 2024 katika mwendelezo wa ziara ya Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya CRB inayofanywa katika mikoa minne ya Kanda ya kaskazini ambayo ni Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga kwa lengo la kukagua utendaji kazi wa makandarasi na utekelezaji wa miradi.

Aidha Mhandisi Joseph Nyamhanga, ametumia fursa hiyo kuzitaka kampuni za kigeni zinazojenga miradi nchini kutoa kandarasi ndogo (sub-contractors) zenye thamani kubwa ya fedha kwa makandarasi wazawa ili miradi hiyo iwajengee uwezo.

Mhandisi Nyamhanga ameyasema hayo wakati Wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya CRB walipotembelea mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika mkoa wa Kilimanjaro wenye thamani ya Shilingi bilioni 18.4 wenye urefu wa kilometa 270 unaotekelezwa na Mkandarasi Ceylex Engineering (PVT) Ltd kutoka Sri Lanka.

Akitoa taarifa kwa wajumbe wa bodi hiyo pamoja na Menejimenti ya CRB, meneja wa mradi Mhandisi Sakina Mohammed amesema kuwa mradi huo wa REA ni wa miaka miwili na utasambazwa katika vitongozi 135 vya mkoa wa Kilimanjaro na mpaka sasa umefikia asilimia 11.6 ya utekelezaji wake.

Katika hatua nyingine Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Menejimenti ya CRB, walitembelea mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi wenye thamani ya Shilingi trilioni 1.4 unaotekelezwa na Mkandarasi China Petroleum Pipeline Engineering Co. Ltd (CPP) katika kijiji cha Misino, wilaya ya Handeni mkoani Tanga na kuridhishwa namna mradi huu unavyotekelezwa.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa mradi huo Mwenyekiti wa Bodi ya CRB, Joseph Nyamhanga amempongeza mkandarasi huyo kwa kuajiri Watanzania kwa zaidi ya asilimia 70 pamoja na kutoa fursa ya kandarasi ndogo (Sub – Contractors) kwa makandarasi wazawa, ambapo pia amewataka makandarasi hao kukamilisha mradi kwa viwango na kwa wakati.

 
Nice kiukweli miradi ya pesa hizo tunaimudu na ubora ni wa hali ya juu. Tunaitaji utekelezaje sasa isiwe tu porojo za kwenye media.
 
Back
Top Bottom