Mwenyekiti wa Bunge la katiba anastahili kutoka CCM tena mtu kama Chenge?

Mwenyekiti wa Bunge la katiba anastahili kutoka CCM tena mtu kama Chenge?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Hivi hawa wana- CCM ambao walikuwa hawana hata agenda ya katiba mpya na waliokuwa vinara wa kupinga wazo hili kweli wanastahili kugombea uenyekiti wa Bunge hili huku mtu kama Chenge anaetajwa akiwa na tuhuma kibao?

Watanzania tuache utani,hakuna mtu ndani ya CCM atakaeweza kuweka mbele maslahi ya Taifa.

Ni kigogo gani kati ya hao wanaotajwa(Sitta na Chenge) anaeweza kusimamia vizuri mchakato huo?

Hata kama mmoja wao ni msafi kidogo,wanaomzunguka je?

Mwenyekiti wa hili Bunge anastahili kuwa na sifa moja kubwa ya kutokuwa kwenye "system" tangu uhuru.

Tofauti na hapo yatakuwa ni yale ya spika Makinda na serikali ya CCM Bungeni.
 
Nikweli bwana salary slip maaanabwana andrew chenge , kwaza kabla hajagombea uenyekiti alitakiwa sisi kama wananchi ,aturudishie mapesa yetu aliyoyakwapua na kuyaficha huko New jessey na vilevile na huko kenye mabenki yaliyopo nchini Uingereza na visiwa vya jirani jamani acha Mungu aje afanye kazi yake malipo nihapahapa duniani .
 
Mwenyekiti wa bunge hawezi kutoka nje ya ccm! Ccm wamejaza wajumbe kutoka kwenye chama chao kwa ajili ya kupiga kura tu na si vinginevyo! Wengi hawana hoja hata kidogo! Watanzania wajue mawazo yao yanaenda kuchakachuliwa mchana kweupe hapo dodoma!
 
Chenge! du watafanya tukose hamu hata ya kuangalia bunge.
 
Hivi hawa wana- CCM ambao walikuwa hawana hata



Ni kigogo gani kati ya hao wanaotajwa(Sitta na Chenge) anaeweza kusimamia vizuri CCM Bungeni.
Kapimwe akili hoja zako mara zote huwa za kijinga!
 
Hana moral authorithy....akipita najitoa rasmi kwenye mchakato unaoendelea. Bora kuendelea na katiba iliyopo
 
Kapimwe akili hoja zako mara zote huwa za kijinga!

We ni agent wa mafisadi tu huna lolote!

Badala ya kujibu hoja unaleta mipasho!

Narudia,mwenyekiti wa hili bunge hastahili kuwa mtu aliekuwa kwenye system muda mrefu.

Wewe kama unafaidika na huu utawala wa hovyo isiwe sababu ya kututaka na sisi wengine tukae kimya!

Chunga domo lako!
 
Mwenyekiti kutoka ccm itakuwa ni sawa na nyani au tumbili kuachiwa shamba la mahindi.
 
Back
Top Bottom