Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 302
MWENYEKITI wa Chama Cha Jamii (CCJ), Richard Kiyabo, amevamiwa na kuporwa mkoba uliokuwa na nyaraka za chama hicho kinachopigania usajili wa kudumu.
Kiyabo, anadaiwa kuwa alivamiwa na watu wanne wasiofahamika na kumpora mkoba wake uliokuwa na nyaraka mbalimbali za chama hicho kilichojizolea umaarufu katika kipindi kifupi.
Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa tatu asubuhi jijini Dar es Salaam katika maeneo ya Kariakoo, Mtaa wa Msimbazi, jirani na jengo la klabu ya soka ya Simba, ambapo Kiyabo alikuwa akitembea kwa miguu.
Baada ya tukio hilo, Kiyabo alitoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Msimbazi na kupatiwa RB yenye namba MS/RB/3606/2010.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, mwenyekiti huyo alisema alishangazwa jinsi tukio hilo lilivyotokea, kwani lilifanywa kwa kushitukiza na watu hao waliokuwa katika gari dogo aina ya Toyota Cresta, ambalo hakuweza kutambua namba zake.
Kwa kweli hadi sasa naona maisha yangu yamo hatarini hii sasa ni mara ya pili kutokewa na tukio la aina hii, leo (juzi) asubuhi nikiwa Kariakoo nikifuatilia masuala ya chama, ghafla nilivamiwa na watu waliovalia makoti meusi na kupora briefcase yenye nyaraka mbalimbali za siri zinazohusu CCJ.
Walionipora walisimamisha gari lao mbele yangu kidogo kisha wakatoka na kunishika mikono yangu, halafu wakairudisha nyuma, nilikuwa naongea na simu, mmoja wao akatoa kitambulisho chenye nembo ya serikali akanionyesha.
Walipomaliza wakachukua begi langu wakaingia kwenye gari lao ambalo sikutambua namba zake, lakini niliona likiwa na vioo vya giza (tinted) wakaondoka zao muda wote watu walikuwa wakipita wakiniangalia, lakini hawakunisaidia, alisema Kiyabo.
Alibainisha kuwa kutokana na kushtukizwa na tukio hilo, hakuweza kuwatambua kwa sura watu walioshiriki uhalifu huo anaouhusisha na harakati za kisiasa, hasa kipindi hiki ambacho chama chake kimekuwa kikifuatilia usajili wa kudumu.
Alisema ingawa tukio hilo lilitokea mapema, lakini hakuna mpita njia aliyejitokeza kumsaidia zaidi ya kumuangalia huku wengine wakiendelea na shughuli zao.
Kwa mara ya kwanza, mwanzoni mwa Februari mwaka huu, Kiyabo alikumbana na vitisho vya kuuawa alivyopokea kwa njia ya simu kutoka kwa watu asiowafahamu, hali iliyomfanya kutoa taarifa polisi.
Muda mfupi baada ya kuvamiwa kwa mwenyekiti huyo wa muda, aliyekuwa Mbunge wa Kishapu kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Fred Mpendazoe, alikuwa kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) akieleza nia yake ya kukihama chama hicho kikongwe na kujiunga na CCJ. Tangu kuanzishwa kwake, CCJ imekuwa ikihusishwa na vigogo kadhaa wa CCM ambao baadhi yao wamekuwa wakikikana chama hicho ambacho katika kipindi kifupi kimeweza kuwa masikioni na machoni mwa wananchi, kutokana na habari zake kuandikwa na kutangazwa mara kwa mara na vyombo vya habari.