Mwenyekiti wa CCM Kagera: Mtaa hauhitaji digrii na PHD na watu wenye vyeti pekee, mtaa unahitaji ujuzi

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kagera, Faris Buruhan, amewataka vijana wanaopata mafunzo ya ufundi katika vyuo vya VETA kutumia vyema ujuzi wao, akisisitiza kuwa ajira mtaani zinategemea zaidi ujuzi na utendaji kazi badala ya vyeti vya elimu ya juu.

Faris ametoa kauli hiyo jana, Machi 12, 2025, alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Karagwe, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 16 mkoani humo.

ccm .png

Amesema elimu ya ufundi stadi ina nafasi kubwa katika maendeleo ya taifa, kwani kinachohitajika zaidi ni maarifa ya kiufundi na uwezo wa kubuni mambo yatakayowawezesha vijana kujiajiri au kuajiriwa kwenye sekta mbalimbali.

"Leo, mtaa hauhitaji digrii, PhD, wala vitabu vingi, bali unahitaji watu wa kuendesha mitambo viwandani. Mpango wa nchi ni kuwekeza kwenye viwanda, na wanaoendesha mitambo siyo wenye vyeti pekee, bali wale wenye maarifa na ujuzi wa ufundi,"

Source: Nipashe
 
Kauli za hovyo hizi za kudunisha umuhimu wa elimu, ujuzi, uzoefu na maarifa
 
Yuko sahihi! Ila yy anaujuzi gani nnje na siasa
 
Hivi huyu mpuuzi mbona anawaibisha ishomile.
 
Naona baada ya PM kuongea Mazezeta yameanza kuchomoza kutoka shimoni....
Bongo ina watu malofa sana asikwambie mtu....
Kila mtu ashinde mechi zake!
 
Back
Top Bottom