Mwenyekiti wa CCM Mbeya kasema kweli. Mpuuzeni na mtaikosa Mbeya

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,207
Reaction score
13,839
Your browser is not able to display this video.

Majuzi katika ziara ya Makamu wa Rais Phillipo Mpango huko Mbeya, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya aliorodhesha miradi mingi ambayo serikali iliahidi lakini haijatekelezwa kwa miaka mingi.

Kuna miradi iliahidiwa na Rais Mwinyi na Jakaya Kikwete wakati wa kampeni za urais, lakini utekelezaji ni sifuri.
AHADI NI DENI.

Marais wakati wa kampeni wanaomba kura na kuahidi hewa. Huo ni utapeli wa kisiasa. Wananchi wa Mbeya tunasimama na Mwenyekiti wa CCM Mbeya kuwa Serikali itekeleze ahadi zake. Kinyume cha hivyo wananchi wanakosa imani na serikali.

Katika hili majibu ya Makamu wa Rais Phillipo Mpango yanamuweka Rais Samia katika nafasi ngumu.

Tunataka utekelezaji wa ahadi, hasa za barabara, nothing less.
 
Naona Filipo Mpango hawaelewi watu wa Mbeya,
They call a spade a spade.
Huwa hawamung'unyi maneno.
Fact kwa fact.
CCM ikipenda utopolo kama waongea hovyo kina Makamba, wataipoteza Mbeya kabisa.
 
Bwana Mpango hakutakiwa kumkanusha Mwenyekiti CCM Mkoa hadharani.
Hata aliposema CCM Hoyee! Walimuitikia ni jukwaa kuu peke yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…