Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Ndugu Shemsa Mohamed, ameshiriki kikao muhimu cha wadau wa biashara ya nafaka pamoja na AMCOS kilichofanyika tarehe 27 Januari 2025 katika Ukumbi wa Bariadi Conference, Wilaya ya Bariadi.
Kikao hiki kiliwaleta pamoja wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo na biashara ya nafaka,Vyama vya Siasa, ambapo masuala muhimu yamejadiliwa kwa lengo la kuboresha sekta ya kilimo na kuongeza tija kwa wakulima na wafanyabiashara wa nafaka.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa aliwahimiza wadau kushirikiana kwa karibu, kuimarisha usimamizi wa vyama vya ushirika (AMCOS), na kuhakikisha kuwa wakulima wanapata masoko yenye tija kwa mazao yao.
Ndugu Shemsa Mohamed alisisitiza dhamira ya CCM ya kuendelea kuhamasisha na kusimamia utekelezaji wa mipango inayolenga kuinua uchumi wa wakulima na kuwawezesha kufikia maendeleo ya kweli kupitia sekta ya kilimo.