Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu turudishie CCM kwenye misingi yake

Wewe ni aina ya CCM wenye akili
CCM ya Napd na Kinana ilikuwa insjibu hoja kwa hoja, CCM hii ya Shaka na mwenzie nani sijui hata nina lake wanategemea virungu vya polisi viwanyamzishe wapinzani!
Hili tutapambana nalo hadi CCM yenyewe irudi kwenye siasa zake
 
Kutumia dola kubaki madarakani sio uimara wa chama
 
Siasa mchezo mchafu sana...

Inawezekana kabisa hili vuguvugu nyuma yake yuko mama, amewafinyia jicho waendelee tu.
 
Haya ndo madhara ya CCM ya sasa, yaani yeyote anayepingana na mwenendo mbaya wa CCM anaonekana sio kindakindaki

Hujui uharisia wa hari ya chama. Tulia na subiri kushangilia ushindi.
 
Hujui uharisia wa hari ya chama. Tulia na subiri kushangilia ushindi.
Huo sio ushindi wa chama cha siasa, huo ni ushindi wa Polisi dhidi ya chama cha siasa (upinzani)
 
Leo ndiyo nimemsoma Mwana CCM ambaye anajua kwa nini TANU ilidai uhuru ili kujitawala.
Pia nimeona kuwa kuna mtu anaweza kusema ukweli daima.
Ila tu niwahakikishie wana CCM kuwa kama Viongozi wa dini zote hapa nchini ambao Mwenyezi Mungu huwa Anajibu maombi yao wakaomba Mwalimu Nyerere akafufuka akaelezwa madudu ya CCM ya sasa hata akasikia kuna mpinzani alipigwa risasi tu acha kuuawa, Nyerere ama hangekubali kuishi Tanzania au angeanza upya kupigania Uhuru! Nadhani wengi mnaelewa ninachosema na mimi sina Chama hapa nilipo ingawa nilikuwa Umoja wa Vijana wa TANu wakati tunagombea Uhuru. Huu ni wakati wa kujisahihisha tusingoje Mwenyezi Mungu aingilie kati. Na Viongozi wa dini waache unafiki na kuganga njaa. Wapiganie ukweli.
 
Acha tu inauma sana. CCM ilipaswa kuwa baba la Vyama vya siasa barani Afrika, lkn kwa sasa sivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…