Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilosa anafisidi mashamba ya ushirika wa miwa

mbikagani

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2014
Posts
3,107
Reaction score
1,782
Habari wanaJF,

Huyu anafahamika kwa jina la Ameir. Ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Wilaya ya Kilosa.

Kama mnakumbuka huyu alishawai kutajwa na waziri wa ardhi mh Lukuvi mbele ya Rais Magufuli kuwa anamiliki mashamba makubwa kinyume na utaratibu.

Kwa sasa amevamia kata inaitwa Mbigiri na kujipatia shamba la ushirika wa miwa(AMCOS) kwa njia isiyosahihi.

Shamba lenye thamani ya milioni mia tisa (Tshs 900,000,000), yeye amepitia njia batiri na kulipata kwa milioni mia tatu (Tshs 300,000,000).

Mbaya zaidi hicho kikundi cha ushirika walishawekeza kwa kuchimba visima vya kumwagilia na kupanda miwa. Yeye kwa kupiti viongozi wa ccm na wa serikali, kwa vile ana nguvu ya kifedha na cheo cha uenyekiti wa chama, anawashurutisha viongozi hawa kuchoma miwa moto na kupora maeneo yao waliyokwisha yalima.

Kimsingi hakuna anayeweza kumgusa huyu jamaa, si mkuu wa wilaya wala watendaji wa wilaya.

Tunamuomba Rais Magufuli ammulike huyu chairman wa wilaya CCM, ni mtu jeuri na kiburi sana.

Kwa kutumia cheo chake na nguvu ya fedha aliyonayo anasabisha shida sana hapa kilosa.

Ameagiza watu wachome moto miwa na alipoitwa bwana shamba na polisi kutoa tathimini ya hasara eneo zaidi ya hekeri ishirini, huyu bwana shamba kaleta majibu ya nil, maana hakuna thamani yeyote.

Ameir ni mtu hatari sana hapa Kilosa kwa upande wa migogoro ya mashamba.

miwa iliyochomwa..jpg
 
Huoni aibu kumtuhumu Mwenyekiti wa Chama?

Kilosa ni mojawapo ambapo CCM ilishinda kwa kishindo kikubwa na idadi ya watu kupita bila kupingwa.

Raila alimtumhumu Uhuru kenyata kuwa familia ya Kenyata ina ardhi kubwa na jibu la Kenyata lilikuwa 'The land was acquired legally through genuine seller and genuine buyer"
 
Kimsingi tunafahamu jinsi wanavyolindana na kuogopana ndani ya chama, but for this illegal capture tutaelewa tu.
Hata hotel ya mr sugu watu wasingepiga kelele ingebomolewa kama walivyokata bustani ya Mbowe.
 
Achana na majungu unapoteza muda na wewe tafuta pesa kwa bidii.
 
Huoni aibu kumtuhumu Mwenyekiti wa Chama?

Kilosa ni mojawapo ambapo CCM ilishinda kwa kishindo kikubwa na idadi ya watu kupita bila kupingwa.

Raila alimtumhumu Uhuru kenyata kuwa familia ya Kenyata ina ardhi kubwa na jibu la Kenyata lilikuwa 'The land was acquired legally through genuine seller and genuine buyer"
Kwamba mwenyekiti wa chama ni malaika akifanya kosa akaushiwe. Nope
 
Mtakoma na CCM yenu, na hizo ndiyo connection mkulu alikuwa anazitaka, ukipata nafasi fisadi na wewe mkuu hakuna namna hii nchi ni shamba la bibi.
 
Huoni aibu kumtuhumu Mwenyekiti wa Chama?

Kilosa ni mojawapo ambapo CCM ilishinda kwa kishindo kikubwa na idadi ya watu kupita bila kupingwa.

Raila alimtumhumu Uhuru kenyata kuwa familia ya Kenyata ina ardhi kubwa na jibu la Kenyata lilikuwa 'The land was acquired legally through genuine seller and genuine buyer"
Wanatakiwa wapigwe haswa mpk wakome, safi sn Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi
 
Mtoa hoja bila shaka nawe unaunga mkono juhudi na unafurahia kwa no 1 kuwa very powerful kama semi God,tungekuwa na taasisi imara ungeenda mahakamani,ungeenda kwa tume ya human rights au kwenye tume ya maadili ya viongozi au kwa public protector,but kwa sasa hizi bado ni ndoto means miaka 5 mingine.
 
Mkuu kama wananchi wa kimara walikuwa na 'stop older' mkononi still wakavunjiwa nyumba zao, itakuwa mkulima wa kawaida kaka.

Tunajaribu kuionyeshea jamii tu jinsi watu fulani walivyo juu ya sheria.
 
Kama wamepora uchaguzi na mkaa kaa kimya, subirini siku akili iwarudie mkianza kuhoji tu mtapotezwa wote.
 
Mwenyekiti wa ccm taifa anafisadi Kodi ya watanzania kwa kujenga international airport Kijijini kwake Chato. Mbona huyu hakamatwi?

Huyo wa Kilosa msimsimange! Nasema uwongo ndugu zangu?
 
A closure system, au siyo!
 
Back
Top Bottom