Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Katavi, Rhoda Kunchela, amewataka wananchi wa mtaa wa Kampuni, kata ya Misunkumilo, Mpanda Mjini, kujitokeza kwa wingi na kufanya maamuzi sahihi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Soma pia: Mwenyekiti CHADEMA Katavi: Mkishapiga kura nendeni kwa Mtendaji mwambieni ukipindua matokeo sisi tunapinduka na wewe!
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kuwanadi wagombea wa CHADEMA kwa nafasi za uenyekiti wa mitaa, Kunchela amewahimiza wananchi kutoacha hali ya kudhoofisha demokrasia iwazuie kuchagua viongozi wenye kujali maslahi yao.
Rhoda alisema yafuatayo:
"Inawezekana vijana wako wote wana kazi, wana ajira, hujawahi kupotelewa na mtoto aliyekamatwa na polisi akasingiziwa kesi, ukaona suala la demokrasia na uchaguzi halikuhusu. Ninawaomba muwe na hasira, mfanye maamuzi ya kueleweka. Mchague CHADEMA, ipiganie CHADEMA, mlinde kura zenu, na polisi wakija msitishike, msitishwe na mabomu," amesema Kunchela.