Naona kama joto la uchaguzi limezidi kuwa la moto na hii ni baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA huko jijini Mbeya kuwavaa CCM na chama chao
Masaga Pius Kaloli akiwa anazungumza leo huko jjini Mbeya amedokeza kuwa wanachama wengi wa CCM wanataka kujiunga na CHADEMA lakini wanaogopa kujiunga na chama hicho kwa sababu wanaogopa kutekwa
"Leo CCM wanajua chama chao ni chama cha wezi. Wanajua chama chao kina makundi ya watekaji. Wanajua. WanaCCM wa nchi hii sio mafala nao wamechoka. Wanaogopa kuja leo CHADEMA kwa sababu mnatisha na kutesa watu, wanaogopa"
Wakuu hivi inawezekana kweli kuna wanaCCM wanataka waingie CHADEMA lakini wanahofia maisha yao?