Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Kauli za kishujaa zinazidi kutawala kutoka kwa viongozi wa CHADEMA. Hii ni kuwajengea kujiamini wananchi katika kipindi hiki cha uchaguzi wasibabaishwe na watu wenyenia ya kuharibu uchaguzi.
==================
Mwenyekiti wa CHADEMA @chadematzofficial Mkoa wa Katavi, Rhoda Kunchela, amesisitiza umuhimu wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa kufanyika kwa haki na amani, huku akionya vikali dhidi ya vitendo vya rushwa vinavyoweza kuathiri uchaguzi huo.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Imilamate, kata ya Itenka, jimbo la Nsimbo, mkoani Katavi, Novemba 24, 2024, Kunchela amehimiza wapiga kura na viongozi wa CHADEMA kuhakikisha rushwa haipati nafasi wakati wa kampeni na uchaguzi.
“Ili uchaguzi huu uwe huru na wa haki, tunahitaji haki itendeke na rushwa isitawale miongoni mwa wapiga kura,” amesema Kunchela.
Soma Pia:
Kunchela amewataka wafuasi wa CHADEMA kuhakikisha kuwa wanakabiliana na wale wote watakaobainika kuvuruga uchaguzi kwa kutoa rushwa, akitoa mfano wa hatua za moja kwa moja dhidi ya wanaojihusisha na vitendo hivyo.
Hotuba yake ni sehemu ya kampeni za chama hicho kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024, ambapo CHADEMA inahimiza usimamizi wa sheria na haki ili kuhakikisha matokeo ya uchaguzi yanawakilisha matakwa ya wananchi.

- Yanayojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Katavi
- Katavi: Mwenyekiti wa CHADEMA: Tunaamini katika haki, maendeleo na kutetea Watanzania kuliko matumbo kama wanavyofanya CCM
- Special Thread: Orodha ya Nyuzi za Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024