Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Kilimanjaro, Gervas Mgonja, kwa madai ya kutoa kauli za kuhamasisha wananchi kuvamia makazi ya wasimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa usiku huu, Novemba 25 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, mtuhumiwa huyo amekamatwa baada ya kuonekana kwenye video mjongeo iliyosambaa katika mitandao ya kijamii, akiwa anawahamasisha wananchi kufanya uhalifu Novemba 27,2024.
PIA SOMA
- LGE2024 - ACT Wazalendo: Tumesikitishwa na kitendo cha Polisi kumkamata Mwenyekiti wetu Mkoa wa Songwe, Ezekia Zambi
"Maneno hayo ya kuhamasisha vurugu, aliyatamka hadharani Novemba 24,2024, na baada ya kutamka waliyasambaza katika mitandao ya kijamii" amesema Kamanda Maigwa.
Aidha, amesema mtuhumiwa anachukuliwa maelezo ili hatua zingine za kisheria ziweze kufuata.
TAARIFA MIKOA MINGINE SOMA
- LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024