Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Hii ndiyo Taarifa ya hujuma mpya inayosambaa mitandaoni kwa sasa , kwamba David Chiduo ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kilosa amekamatwa na kuwekwa selo kwa Tuhuma za kuhamasisha maombi kwa wanachama wa Chadema wa Wilaya hiyo kwa ajili ya kumuombea Freeman Mbowe , aliyewekwa gerezani na watawala wa Tanzania kwa tuhuma za uzushi za Ugaidi .
Ikumbukwe kwamba OCD wa Kilosa ni ndugu Lwelwe Mpina aliyekuwa OCD wa Hai na ambaye alishirikiana na Ole Sabaya kwenye masuala yote ya ujambazi wa kutumia Silaha na uporaji , badala ya Lwelwe Mpina kuunganishwa kwenye kesi za Sabaya , akahamishwa na Sirro ili akajifiche Kilosa , ambako bado anaendeleza unyama ule ule alioufanya Hai akijiamini kwamba ataendelea kulindwa .
Mungu ibariki Chadema