Mjue Mwanasiasa Mtanzania
Member
- Aug 21, 2021
- 16
- 20
BARUA YA WAZI KWA MHE RAIS SAMIA SULUHU HASSAN
Mh Rais Pole Kwa majukumu, Mimi naitwa Emanuel Magoya Lucumay ni mkazi wa jimbo la Hai, nimelazimika kuandika barua hii kuelezea kilio cha familia yetu ya Ukoo wa Magoya juu ya manyanyaso tunayopitia, dhuluma Kubwa tuliofanyiwa na Emanuel Loishyie Laiza na Rafiki yake Edmund Rutaraka ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Halmashuri ya Hai.
Mh Rais, Ndugu watajwa hapo juu ni watu wakihusika kumdhulumu ardhi yenye ukubwa wa hekeri 20 baba yangu Lucumay Magoya anaepatikana Kitongoji Cha Mlima Shabaha Kata ya Muungano.
Dhuluma hii imefanywa na Ndugu Loishyie Laiza akisaidiwa na Diwani wa kata yetu ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri yetu, tumejaribu kushtaki Kwa Mwenyekiti wa Kitongoji Ndugu moseka Singo bila mafanikio, tumefikisha Kwa Mwenyekiti wa ccm kata ndugu Dave bugama lakini nae ameshindwa kulitatua maana Mwenyekiti wa Halmashauri amekuwa anawatisha watumishi wa Halmashauri wanaoonyesha kutaka kutusadia, na Jana wametuma Mjumbe wa Kijiji aje kututisha kuwa tukiendelea kufuatilia suala hilo atatupoteza.
Mhe Rais Tunaomba uingilie kati jambo hili, najua kesho utapita hapa Kwa sadala naomba niongee hili hadharani, tumechoka manyanyaso ya Mwenyekiti Rutaraka ambae amekuwa akiwatumia marafiki wake matajiri kupora ardhi za wanyonge.
Malalamiko dhidi ya Mwenyekiti Huyu yamekuwa mengi sasa, anatisha watumishi wa umma waadilifu, anatisha wafanyabiashara, ameunda Magenge mitandaoni yakutukana serikali na viongozi wa Chama ambao wanajaribu kumsahihisha na kumshauri.
TUSAIDIE MAMA, HUYU MWENYEKITI ONDOKA NAE MAMA.