OgwaluMapesa
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 10,942
- 434
Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania na Mhariri Mtendaji wa New Habari, Ndugu yetu Absalom Kibanda anarejea kesho saa saba mchana na ndege ya SAA kutoka kwenye matibabu ya muda mrefu nchini Afrika Kusini baada ya kutekwa na watu wasiojulikana nje ya nyumba yake akirudi nyumbani siku 88 zilizopita na kuumizwa vibaya sana na kuachwa kufa.
Watanzania wote wenye nia njema ya kumpokea na kumfariji, tujumuike pamoja kesho uwanjani JK Nyerere international Airport.
============
Watanzania wote wenye nia njema ya kumpokea na kumfariji, tujumuike pamoja kesho uwanjani JK Nyerere international Airport.
============
| MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda anatarajia kuwasili leo akitokea nchini Afrika Kusini alipokuwa akitibiwa tangu Machi 6, baada ya kushambuliwa na kuumizwa vibaya na watu wasiofahamika usiku wa Machi 5. Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa TEF, Neville Meena, Kibanda atawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere leo saa 7 mchana na atazungumza na waandishi wa habari. Kutokana na ujio huo, Meena aliwaomba wahariri na waandishi kufika uwanjani hapo kuanzia majira ya saa 6.00 mchana kwa ajili ya kumpokea mwenzao huyo aliyekaa nje ya nchi kwa miezi mitatu. Mwenzetu kakaa Afrika Kusini kwa siku 90, hii ni fursa nyingine adhimu ya waandishi wa habari nchini kuonyesha mshikamano na umoja wetu kwa kwenda kumpokea, alisema. Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd, kuumizwa kwake kuliitikisa tasnia ya habari nchini na kuzua mijadala mbalimbali ndani na nje ya nchi. Tukio lilivyotokea Ilikuwa usiku wa Machi 5, ambako Kibanda alijikuta ametekwa na watu wasiofahamika na kisha kumjeruhi vibaya kwa nondo, mapanga na kisha kumngoa meno, kucha na kumharibu jicho la kushoto. Tukio hilo la kinyama ambalo lilifananishwa kwa kiasi fulani na lile alilofanyiwa Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania, Stephen Ulimboka, lilitokea wakati Kibanda akiwa anarejea nyumbani kwake Goba Punguni, Kata ya Mbezi Juu, baada ya kutoka kazini. Kutokana na kuumizwa vibaya, Jukwaa la Wahariri kwa kushirikiana na wadau wengine wa habari walilazimika kufanya taratibu za kumsafirisha kwenda Afrika Kusini kwa matibabu zaidi ambako pia alisindikizwa na daktari kutoka Taasisi ya Mifupa Muhimu (Moi). Awali akielezea tukio lilivyokuwa, Kibanda alisema: Nilifika nyumbani kwangu kama saa sita usiku nikitokea kazini na nilipofika kwenye lango la kuingia ndani nilipiga honi ili mlinzi anifungulie. Lakini ghafla nilivamiwa na kundi la watu ambao walivunja kioo cha gari langu upande niliokuwa nimekaa. Nilitokea kupitia mlango wa abiria, lakini sikuweza kuwakimbia watu wale kwani walinikamata na kuanza kunishambulia kwa vitu vizito. Baada ya kutoka kwenye gari, nahisi nilikanyaga sehemu mbaya, nikateleza na kuanguka wakanifuata... niliona kama watu watatu hivi wakaanza kunishambulia. Sikuwa nafahamu kilichojiri, lakini nilisikia mwingine akimwambia mwenzake afande mshuti... mshuti. Huyo alipoelekeza mtutu na kujaribu kushuti (kupiga risasi) ilikuwa kama vile imegoma. Nikiwa bado niko chini, wakanipiga kwa kitu cha ncha kali kwenye jicho la kushoto, wakaningoa meno na kucha katika vidole vya mkono wa kulia, walinipiga sana na nilipata maumivu makali. Baada ya kunipiga na kunijeruhi waliniburuza hadi pembeni ya nyumba yangu na kunitupa na wakaondoka, baadaye majirani na wasamaria wema walikuja kuniokoa. PIA, SOMA: - Absalom Kibanda (Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri) avamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa |
