Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Ruto aitisha kikao cha dharura ndani ya saa 48 kujadili mapigano ya Congo na Rwanda

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Ruto aitisha kikao cha dharura ndani ya saa 48 kujadili mapigano ya Congo na Rwanda

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Rais wa Kenya William Ruto ametangaza kufanyika kwa mkutano na viongozi wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kuhusiana na mgogoro katika eneo la Mashariki mwa DRC, ambao utafanyika katika siku mbili zijazo.

Ruto alishukuru Rais wa DRC, Etienne Tshisekedi, na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kwa kukubali kuhudhuria Mkutano huo wa kipekee wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) utakao fanyika katika kipindi cha masaa 48 yajayo.

Pia soma
- Jumuiya ya Afrika Mashariki imzuie Kagame kunywa damu ya wakongo, na kula nyama zao katika vita ya Mashariki mwa Kongo
 
Kiongozi wa Waaasi bwana Cornelle Nangaa aliunda umoja wa makundi ya Kisiasa na Kijeshi unaitwa Alliance for Congo River ambapo wanachama wao ni pamoja na M23 Wakiwa Nairobi Kenya Hadi DRC kulalamikia na kupelekea Jeshi la Kenya la kulinda amani kufurushwa.

Huyo Nangaa akiwa Mkuu wa Tume ya Uchaguzi na mashirika wa Kabila ndio walimpa Urais Felix Tschisekedi baada ya kumpora Ushindi Martin Fayulu ila baada ya kukosana wakaingia msituni Kwa kulinganisha makundi yote yenye silaha huko Eastern DRC yakiongozwa na M23 Ili kumpindua Tschisekedi Kwa madai kwamba yeye ndio chanzo Cha migogoro
Screenshot_20250128-110201.jpg
Screenshot_20250128-110225.jpg

.https://www.africanews.com/2023/12/15/drc-corneille-nangaa-joins-forces-with-m23-to-create-political-platform/

My Take
Kenya ni mnafiki na sidhani kama DRC itashiriki mkutano wa kipuuzi kama huo ambao unaongozwa na kibaraka https://www.reuters.com/world/afric...rned-rebel-boss-builds-insurgency-2025-01-27/
 
Ruto Mnafiki Mkuu ana hatarisha sana wakenya uko Congo pamoja na biashara zao. Kagame ni mhuni hakika.
 
Back
Top Bottom