Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi Taifa Fadhili Rajabu Maganya ametahadharisha vyama pinzani kuwa chama chao hakiendi kirahisi wala kuonea huruma mpinzani aliye dhaifu katika uchaguzi wa mwaka huu (2025) kwa kuwa wamejipanga kikamilifu kuendelea kushika dola.
Maganya ameeleza hayo mjini Makambako mkoani Njombe wakati akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mara baada kupokewa kwa ziara ya siku tatu mkoani humo.
"Tunataka tuwapige kweli kweli, hatuwezi kuchukua mambo kirahisi kwa hiyo tuwaambie vyama rafiki tunataka tutumie silaha nzito na za kisayansi kuhakikisha tunawashinda kitakatifu na hatutajali kwamba tutumie silaha gani, sisi tutatumia bomu kuua nzi" amesema Maganya
Amewataka wanaCCM kutokuwa na wasiwasi na kwenda kuisemea vizuri serikali kwa kuwa imetekeleza kikamilifu Ilani yao.
Aidha Maganya amesema Chama cha Mapinduzi hakikutaka kuchelewa kumtangaza mgombea wao wa Urais ili kuwa wanachama utulivu wa akili ili kufikilia namna ya kutekeleza Ilani nyingine ya uchaguzi ya mwaka 2025-2030.