Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala (CCM) na Mbunge, acheni vurugu na kuharibu chama

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala (CCM) na Mbunge, acheni vurugu na kuharibu chama

Chipoku

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2011
Posts
254
Reaction score
181
CCM kiko katika chaguzi zake za ndani (kuanzia ngazi za mashinq, Malawi, Kata, Wilaya, na Mikoa) nchi nzima katika kipindi hiki. Ni Utaratibu mzuri wa Chama Tawala uliojiwekea ambapo wanachama wake katika maeneo husika hutumia fursa hii ya kidemokrasia ndani ya chama kugombea nafasi mbalimbali.

Wakati zoezi hili linaendelea hususan katika ngazi za matawi kumekuwa na vurugu za hapa na pale zinazopelekea kukitia Chama Aibu na fedhea.

Wakati uchaguzi wa Jumuia matawini Jimbo la Ukonga unaendelea, Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya amekuwa AKILETA WAGOMBEA MAMLUKI KATIKA MATAWI AMBAO ANATARAJI WAMBEBE 2025 KTK MBIO ZA UBUNGE UKONGA.

Kadhia hii ya Mwnyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya Ilala imeshasababisha fujo, vurugu na sintofahamu nyingi; SABABU HUJIFANYA KWAMBA HAO WATU WAPITISHWE KWANI NI MAAGIZO KUTOKA JUU; JUU WAPI?

Amesababisha vurugu katika Chaguzi za Jumuiya za Wazazi na Wanawake katika Kata ya Majohe na kusababisha watu kupigana, Mzambarauni nako watu wameumizana, Tawi la sabasaba, Kipunguni A na B nk.

Huyu jamaa na mwenzake Mbunge wanaharibu na kukitia aibu Chama Tawala.

Wamefanya SIASA ya Jimbo la Ukonga imechukua sura mpya sana katika awamu hii. Tumerejea hatua nyingi nyuma katika kuheshimu misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, utawala bora na Uhuru binafsi. Hatuna tofauti na tawala na Vyama vya KIBABE . Wanaipeleka CCM Ukonga na Ilala sehemu mbaya.

Tusikubali mambo haya KUENDELEA BILA KUWADHIBITI WAHARIBIFU HAWA maana nguvu ya ushawishi na uimara wa CCM utapungua au kuyumba.

Makalu Mwenyekiti wa CCM Bara @Abdurahmani Kinana alipatq kusema kuwa "tusikubali wanachama wakaona siku hizi haki na uhuru hakuna au wananchi wakaona chama walichokiheshimu na kukiamini hakiwasikilizi tutajiweka kwenye hatari."

Viongozi mlifanyie kazi hili
 
Back
Top Bottom