KERO Mwenyekiti wa Mtaa wa Kambarage, Kata ya Igogo - Nyamagana ananyanyasa sana Wafanyabiashara, kuwafungia biashara zao bila sababu

KERO Mwenyekiti wa Mtaa wa Kambarage, Kata ya Igogo - Nyamagana ananyanyasa sana Wafanyabiashara, kuwafungia biashara zao bila sababu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
1000099274.jpg
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kambarage, Kata ya Igogo, Wilaya ya Nyamagana amekuwa akiwafungia na kuwaamuru Wafanyabiashara kufunga biashara zao akitumia nguvu bila sababu za msingi.

Amekuwa akitumia Kundi la Askari wa Jeshi la Mgambo pamoja na Askari Jamii, wakiwafungia Wafanyabiashana maduka yao kimabavu huku akiwaomba fedha ili wasifungiwe maduka yao na wakigoma huwakamata kwa nguvu na kuwafungia kwenye chumba kilicho karibu na ofisi yake kwa muda.

Amekuwa akifanya hivyo mara kwa mara hali inayoathiri biashara za Wafanyabiashara kwa muda mrefu kwenye mtaa wake.

Pia, amekuwa akiwaamuru Wafanyabiashara kufunga maduka yao pindi anapoitisha mikutano na Wananchi wa mtaa huo mara kwa mara.

Tunaomba Serikali ngazi za juu itusaidie kwa hilo.

====================

MWENYEKITI ANAELEZEA TUHUMA HIZO
JamiiForums
imewasiliana na Mwenyekiti wa Mtaa wa Kambarage, Peter Kiberenge anaelezea kuhusu madai hayo:

“Inawezekana kuna mtu au Watu wanatumia jina langu, hilo jambo sijafanya na silifahamu, mimi ambacho nimekifanya ni kukutana na Wananchi na kuwakumbusha wakamilisha mchakato wa malipo ya majengo yao na sio vinginevyo.

“Lakini kwa kuwa umeniambia hilo, naomba nilifanyie kazi inawezekana lipo na linafanywa na Watu wanaotaka kunichafua kisiasa.”
 
Back
Top Bottom