DOKEZO Mwenyekiti wa Mtaa wa Mpululu maeneo ya Kikuyu East, Dodoma, anawapora wananchi ardhi kisha anatoa vitisho, Mamlaka zitusaidie

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mawele

Senior Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
119
Reaction score
320
Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa Mpululi, Dodoma anagawa anawapora ardhi Wananchi wanyonge kisha anawapa vitisho

Mtaani kwetu tuna Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa ambaye amekuwa akiwaliza watu wengi sana kwenye masuala ya viwanja, anachukua maamuzi ya kuuza viwanja vya watu hawa wale ambao wanakuwa hawajarejea kwenye maeneo yao kwa muda.

Mbali na hapo amekuwa akiwatisha Wananchi hasa wale ambao hawana uelewa kuwa wakienda kushtaki Jiji kibao kitawageukia na watanyang’anywa viwanja.

Nimesema hayo kwa kuwa yametukuta na sisi kupitia bi mkubwa wangu, kiwanja ambacho mama aliachiwa na mzee wake ambaye ni babu yangu mimi, kuna ndugu wa bi mkubwa ambao walishea mama (hawahusiki kabisa na kiwanja cha babu yangu) wanacheza dili na Mwenyekiti ili wachukue kiwanja cha mama yangu.

Mwenyekiti huyo ni wa Mtaa wa Mpululu maeneo ya Kikuyu East, Dodoma, anaitwa Kenneth Makoso.

Mwenyekiti huyo anashirikiana na Watu kadhaa ambao akichapewa chake tu basi anaingilia kesi za ardhi hata ambazo hazimuhusu na kujifanya yeye ndiye Mahakam ana eye ndiye Hakimu.

Tunaomba Serikali ya Dodoma kupitia Viongozi wa Ardhi, Wizara ya Ardhi pia kutusaidia na kuondoa watu wa aina hii, kwani wao ndio chanzo cha kutengeneza migogoro mingi kwenye Jamii.

Anagawa maeneo ya ardhi yanayomilikiwa na Mama ambaye amekuwa akimiliki tangu Miaka ya 1990 alipoachiwa na babu Kiwanja tangu Miaka ya 1990, anafanya hivyo kwa kuwa mama anaishi Dar es Salaam na hapo amekuwa akiendelea ujenzi mdogomdogo.

Sisi ambao hatujuani na Watu Serikalini tunakandamizwa haki zetu, inauma sana.
 
Kafungueni kesi kitengo Cha ardhi
 
Back
Top Bottom