ghilipolla
JF-Expert Member
- Jan 6, 2014
- 280
- 53
Nakuwa nikifuatilia Bunge kwa makini sana na uongozi wa Mwenyekiti wa Muda Bungeni Pandu Ameir Kificho nimegundua huyu mzee anastahili sifa japo wachache walibeza kuchaguliwa kwake kutokana na sifa zake kielimu. Nikijaribu kumlinganisha na Spika wa Bunge wa JMT wa sasa nakuta kuna tofauti kubwa sana, huyu mzee sijawahi kumuona akikasirika pale mbunge anapolazimisha kuomba mwongozo wala kwa vyovyote hutumia busara sana na ile misisimko bungeni huwa inatulia automatically. Huwa namhisi anajaribu mtu kuomba mwongozo au taarifa au ombi basi mara nyingi hutoa ile nafasi na si mara nyingi kumkatisha mtu wakati anaongea. kwenu wakuu munalionaje hili