Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,972
UME ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imeitaka CCM) kungoa mabango ya picha za mgombea wake wa urais, Jakaya Kikwete zilizopigwa kwenye maeneo ya Ikulu.
Mwenyekiti wa Nec, Jaji Lewis Makame aliliambia gazeti hili jana kuwa agizo hilo pia linavihusu vyama vyote vilivyotumia mabango ambayo hayakuthibitishwa na tume hiyo.
Tumeshaviagiza vyama vyote vinavyotumia mabango ambayo hayakupitishwa na Nec viache mara moja, alisema Jaji Makame ambaye tume yake ilikutana kwa siku mbili mwishoni mwa wiki kujadili suala hilo lililoibuliwa na Baraza la Ushauri la Vyama vya Siasa.
Lakini agizo hilo si kwa CCM tu, bali vyama vyote vinavyotumia bango ambalo halikuhakikiwa na tume.
Mwananchi iliripoti mwishoni mwa wiki kuwa Nec ilijadili suala hilo kwa siku mbili mfululizo na kuwahoji wawakilishi wa CCM kuhusu baadhi ya mabango yanayomuonyesha mgombea wake wa urais akiwa Ikulu.
Gazeti moja la kila siku la Kiingereza liliripoti jana kuwa chama hicho tawala kilianza kuondoa mabango mawili makubwa ya barabarani yaliyowekwa mkoani Kagera, ikitii sheria za nchi baada ya mabango hayo kutopitishwa na Nec.
Gazeti hilo linamkariri katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba akisema kuwa chama chake kinaheshimu sheria za nchi. Makamba alionekana kwenye kituo cha televisheni cha TBC akisema kuwa mabango yote ya CCM yalishapitishwa na Nec na kwamba wanafanya kazi kwa makini.
Lakini baada ya vikao vya siku mbili mfululizo, CCM ilianza kuondoa mabango hayo hata kabla ya taarifa rasmi ya Nec jana.
Jana, Makamba hakutaka kuzungumzia suala hilo baada ya Mwananchi kumpigia simu kutaka ufafanuzi.
"Mimi niko Bumbuli kwenye mikutano ya kampeni za mwenyekiti. Kama taarifa hiyo ipo nitaikuta ofisini, nisubiri," alisema Makamba.
Sakata la mabango lilianza Septemba 6 mwaka huu wakati Baraza la Ushauri wa Vyama vya Siasa lilipoitaka CCM kutotumia picha zilizopigwa Ikulu katika mabango ya mgombea wake wa urais.
Picha za kampeni za CCM zinazoonyesha Ikulu zisitumike, ukitumia hizo picha halafu chini yake ukasema chagua chama fulani, hiyo itakuwa siyo demokrasia kwa sababu hata aliyepiga hizo picha ni mfanyakazi wa Ikulu, alisema Tendwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika mkutano wa baraza hilo.
Kwa mujibu wa Tendwa, picha hizo pia zinawashawishi wananchi kukipigia kura chama hicho wakati vyama vingine haviwezi kupata fursa ya kutumia maeneo hayo kwa kuwa havijashika dola.
Tendwa aliwaeleza waandishi wa habari kuwa mabango hayo ni yale yanayoonyesha picha za majengo ya ofisi na makazi hayo ya mkuu wa nchi.
Hivi karibuni, Naibu katibu wa elimu ya mpigakura na habari wa Nec, Ruth Masham alilieleza gazeti hili kuwa suala hilo lilijadiliwa na Nec kwa kwa siku mbili kabla ya kupata muafaka ambao Makame aliubainisha jana.
Source: MWANANCHI.