KERO Mwenyekiti wa Serikali ya Mitaa Vijibweni Kigamboni anauza kiholela hifadhi ya barabara na kusababisha migogoro ya ardhi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Eneo la Vijibweni kumeongezeka migogoro ya ardhi kwa kuwa mwenyekiti wa Serikali anauza maeneo ya hifadhi ya barabara akishirikiana na kikundi cha wajanja.

Na kumekuwa na malalamiko mengi juu ya huyo Mwenyekiti wa Serikali ya Mitaa na kila anapofuatwa yeye hukimbia ofisi na kutokomea mara kwa mara .

Kuna eneo la hifadhi ya barabara wamemuuzia mtu na kajenga na hivyo kutokuzingatia maadili ya kazi .
Pembeni ya tenki la maji ni barabara na mtu kauziwa.

Tunaomba mamlaka husika walichukulie hatua za haraka kwani kuwekuwa kero na watu wachache kutumia vyeo vyao katika kufanyauhalifu huu.

 
Hapa na kwenye maeneo ya wazi ndio mfereji wa wenyeviti kupiga pesa.
 
Pia anauza maeneo ya wazi kwa kuanza kubadilisha matumizi yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…