Mwenyekiti wa Simba SC Mangungu, CEO Barbara, Kocha Mkuu Pablo, Msaidizi Matola, Mratibu Abbas na Meneja Rweymamu ondokeni Klabuni imetosha

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Nina Taarifa za kutosha tu na za uhakika kuwa Mmoja wenu hapa (kwa niliowataja) kupitia Mdogo wako anatumika kwa Kushirokiana nawe ili Kuihujumu vibaya Simba SC kwa Ahadi ya Kusaidiwa na Kiongozi Mstaafu mwenye Ushawishi katika Utawala wa sasa (wa Mama) ambaye anammudu ili uteuliwe Ubunge.

Kuna Watu wengine Wawili hapa (niliowataja) Wao Kazi yao Siku zote ni Kuiumiza Simba SC kwa kutoa Siri za Kambi ya Simba SC kisha mnalipwa Pesa ya maana na Kampuni ya Tapeli wa Mjini.

Kuna Mmoja hapa (kwa niliowataja) Yeye huwa hataki Ushauri, huwatukana hovyo Wachezaji, huwagawa na hajawahi kujua Kupanga Kikosi chake na hata Timu ikizidiwa huwa hana Plan B na anachojua ni Kufokafoka tu na Pua yake Kubwa iliyochongoka kama barabara ya Sinza Shekilango.

Kuna Mmoja hapa (kwa niliowataja) mara mbili alitahadharishwa kuwa lazima atenge pembeni Hela ya Unyangindo (Utamaduni wa Mwafrika) ila chenyewe na "Kilivyokondeana' kama Miwa ya Kigoma kikakataa halafu baada ya Fei Toto 'Kutufeisha' na Goli langu bora la Michuano ya ASFC haraka mno Kikaomba Radhi kwa wenye Uchungu na Simba SC yao.

Kuna Mmoja hapa (kwa niliowataja) tema huyu ningekuwa nae karibu ningezichapa nae kwa Kunikera kwani pamoja na kupenda kunyoa Para lake baada tu ya Kibu Denis (aliyekuwa ndiyo Kabeba Hirizi ya Simba SC) kugongana na Kibwana Shomary (ambaye nae pia ndiyo alibeba Hirizi ya Yanga SC juzi) alipigiwa Simu mara 17 ya Kumtoa nje Kibu Denis ili 'Unyangindo' ukamilike kupitia 'Jini' letu na Goli lirudi na hata tuongeze lingine hakusikia na kuona haitoshi akazima kabisa na Simu yake.

Ondokeni haraka sana Simba SC yetu.
 
Ha ha ha ngoja waje, ila paragraph ya mwisho inachekesha ya wabeba majini kibu &kibwana
 
wewe nani, na umefanya nini? au upo kwenye keybord yako kulaumu watu wanaohangaika kucha kutwa kwa hali na mali kwa ajili ya timu
 
Helo popoma unawapopoma Simba sc
Mijitu unajitoa kabisa kwa kuipenda Klabu na kuwaambia Yanga SC wamefanya nini ili Kutumaliza lakini hawasikii na Wanatupuuza halafu baada ya Kipigo ndiyo wanajifanya Kusikitika na Kutupigia Simu za Kukiri kuwa walikosea Kutotusikiliza tuliozaliwa Mjini (Watoto wa Mjni) na Wao Washamba (Mambwiga) waliokuja Dar es Salaam na Treni za TRC na Malori ya Ng'ombe kujifanya wanajua na wangewaweza Yanga SC Juzi.
 
Matola na yule meneja kwa sura tu ,unajua kabisa watu wa dili
Hawa Watu Wawili wametuumiza sana Simba SC kwakuwa wanatumika na Watu Wawili Maarufu wa Kundi la Friends of Simba ambao wana Hasira na Mo Dewji pamoja na CEO Barbara kuwatosa katika Dili lao la Kuuza Jezi za Simba SC na Dili kupewa Fred Ngajilo ( alias ) Vunja Bei.
 
Wewe bhana kama una uwezo, lete hela ya kutosha ili nikupe dawa ya kwenda kunyunyizia kwa siri kwenye ofisi zao. Nakuahidi utaona matokeo baada ya wiki moja tu. Wote watazikimbia hizo ofisi zao, pasipo kupenda.

Hata kama kuna baadhi ya wachezaji hupendi wabakie hapo klabuni kwenu msimu huu, wewe njoo tu! Nao utashangaa wanaomba ruhusa kwenda kwao, na kamwe hawatorudi tena klabuni. Ni hela yako tu. Karibu sana Kwa Msisi Handeni Tanga.
 
H
Hili jamaa bwana limejaa kiherehere na umbea tu. Duniani uliwahi kuona wapi timu isiyofungwa? Yaani kukosa ubingwa mara moja ndani ya miaka mitano ndio unatoka povu lote hilo? Huna lolote mbwatukaji mkubwa wa matusi wewe.
 
Simba ipi ifanyiwe hujuma? Ya Mzamiru Yassin na Lwanga?


Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
makolo nguvu moyaaaa
 
Ndio uyu anaeropoka redio leo sio utazan sio timu yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…