Pre GE2025 Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi: Ukijiandikisha mara 2 ili kupiga kura, adhabu ni jela kuanzia miezi 6

Pre GE2025 Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi: Ukijiandikisha mara 2 ili kupiga kura, adhabu ni jela kuanzia miezi 6

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wanabodi,

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Jacobs Mwambegele, amesisitiza kuwa kujiandikisha zaidi ya mara moja ni kosa la jinai lenye adhabu ya kifungo cha angalau miezi sita, kisichozidi miaka miwili, au vyote kwa pamoja.

Ameyasema haya wakati wa mkutano na wadau wa uchaguzi mkoani Tanga, ulioshirikisha viongozi wa serikali, vyama vya siasa, taasisi, dini, na kimila. Vituo vya uandikishaji vitafunguliwa saa 2 asubuhi na kufungwa saa 12 jioni.

Zoezi la uandikishaji wa daftari la wapiga kura litaanza Februari 13 mwaka huu katika mikoa ya Tanga na Pwani na litadumu kwa siku saba.


tume.png

Source: East Africa Radio
 
Back
Top Bottom