MwanaDiwani
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 5,536
- 2,266
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha baraza la katiba wilaya ya Singida wakinyanyua mikono juu kuomba nafasi ya kutoa maoni yao kuhusu uboreshaji wa uundwaji wa katiba mpya. (Picha zote na Nathaniel Limu).Na Nathaniel LimuMwenyekiti wa tume ya rasimu ya katibaAli Saleh Ali, amewataka wajumbe wa mabaraza ya katiba ngazi za wilaya wasiongozwe na ‘mawazo fungwa' wakati wa kutoa maoni yao kuhusu uboreshaji wa rasimu ya katiba.Ali ametoa tahadhari hiyo baada ya kutokea mvutano mkali kati yake na baadhi ya wajumbe wa baraza la katiba wilaya ya Singida, wanaohudhiria kikao cha baraza la katiba kinachoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha wananchi.
Mvutano huo ulisababishwa na baadhi ya wajumbe kudai kuwa mwenyekiti huyo, alikuwa akifanya utetezi mkubwa ulioonyesha kila dalili kwamba una ushawishi wa moja kwa moja wa kutaka wajumbe hao wapitishe kila kitu kilichomo kwenye rasimu ya katiba.
Baada ya kubanwa, mwenyekiti Ali alisema "wajumbe naona mmekuja hapa tayari mkiwa na ‘mawazo fungwa' kitu ambacho kinasababisha tushindwe kuelewana".
Bila kufafanua zaidi juu ya mawazo hayo fungwa, mwenyekiti huyo amesema kuwa kwa utaratibu mjumbe anayeuliza swali ni lazima ajibiwe papo hapo, lakini kwa upande wa maoni, yanachukuliwa kama yalivyo na kupelekwa mbele.
Ali amesema kwa sababu kuna wajumbe waliokuja na mawazo fungwa, wanapata taabu ya akuafikiana na majibu anayoyatoa.
Amesema "Kwa kifupi ni kwamba hakuna maoni ya mjumbe yeyote yatakayoachwa au kukataliwa, mnayo fursa kubwa kila mjumbe kueleza maoni yake anayoona yatasaidia kupata katiba ya ustawi wa kizazi cha sasa na kile kijacho".
Mmoja wa wajumbe wa kikao hicho Elia Digha, ametoa duku duku lake kwamba tume ya katiba imekuja Singida kukusanya maoni na si kutetea rasimu kama alivyoonyesha mwenyekiti.
Digha amesema "Ninyi tekelezeni majukumu yenu yaliyowaleta Singida ambayo ni kukusanya maoni na kuyafikishwa kule yanakotakiwa, mkianza kutetea kile kichopo kwenye rasimu ya katiba, mtakuwa hamtutendei haki".
Katika hatua nyingine, asilimia kubwa ya wajumbe wa kikao waliungana na Watanzania wengine wanaopinga kuundwa kwa serikali tatu.
Wamedai kuwa serikali tatu italeta madhara mengi ikiwemo gharama kubwa ya uendeshaji na pia itachangia kuzorota kwa undugu uliojengeka kwa miaka mingi.
Aidha, wamepinga kipengere cha kuruhusu wagombea binafsi kwa madai utachangia mafisadi kutumia mwanya huo kupata uongozi.
Kikao hicho kilitarajiwa kuendelea tena leo tarehe 26/7

Mwenyekiti wa tume ya katiba Ali Saleh Ali akitoa ufafanuzi juu ya ushiriki mzuri wa kutoa maoni ya uundwaji wa katiba mpya kwa wajumbe wa baraza la katiba la wilaya ya Singida. Kushoto ni mjumbe wa tume ya katiba Jesca Mkuchu.
Mjumbe wa baraza la katiba wilaya ya Singida Elia Digha akitoa maoni yake juu ya uboreshaji wa uundwaji wa katiba mpya kwenye kikao cha baraza la katiba la wilaya hiyo.
Mjumbe wa baraza la katiba wilaya ya Singida Rabeka Itonye akichangia kutoa maoni yake juu ya uundwaji wa katiba mpya kwenye kikao cha baraza hilo.
Mjumbe wa baraza la katiba wilaya ya Singida Elia Digha akitoa maoni yake juu ya uboreshaji wa uundwaji wa katiba mpya kwenye kikao cha baraza la katiba la wilaya hiyo.
Mjumbe wa baraza la katiba wilaya ya Singida Rabeka Itonye akichangia kutoa maoni yake juu ya uundwaji wa katiba mpya kwenye kikao cha baraza hilo.