figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Tarime. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) Wilaya ya Tarime, Godfrey Francis atapandishwa kizimbani muda wowote leo Julai 2, 2018 baada ya kukamilika kwa mahojiano na polisi.
Francis anatuhumiwa kutoa taarifa za uwongo katika mitandao ya kijamii kuhusu sakata la kukamatwa kwa mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Zakaria, Peter Zakaria.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe amethibitisha kukamilika kwa mahojiano ya awali kuhusu tuhuma zinazomkabili kiongozi huyo na kusema atasomewa mashtaka wakati wowote kabla ya shughuli za mahakama kumalizika leo.
"Kweli tutamfikisha mahakamani kujibu tuhuma dhidi yake. Kazi ya Polisi ni kuhoji, kupeleleza na kufikisha mahakamani tuhuma zozote za jinai. Tumetimiza na kukamilisha wajibu huo," amesema Kamanda Mwaibambe.
Kiongozi huyo ambaye juzi alihojiwa na polisi kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana tayari yuko katika ukumbi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Tarime akisubiri kusomewa mashtaka.
Akizungumza na MCL Digital leo Julai 2, Francis amethibitisha kuwa alitakiwa kuripoti polisi leo na alipofika akaelezwa kuwa anapelekwa mahakamani.
"Ndio hivyo nasubiri kusomewa mashtaka; natuhumiwa kusambaza taarifa za uongo kupitia mitandao ya kijamii kuhusu tukio lililomtokea Zakaria (Peter Zakaria). Tunamsubiri hakimu bado ana mashauri mengine," amesema Francis.
Habari zaidi, soma=>Tarime, Mara: Mmiliki wa mabasi ya Zacharia awapiga risasi maafisa wa Usalama wa Taifa, ashikiliwa na Polisi
Chanzo: Mwananchi
UPDATES:
Tarime. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) Wilaya ya Tarime, Godfrey Francis leo Jumatatu Julai 2, 2018 amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Tarime, kushtakiwa kwa kosa la kusambaza taarifa za uwongo kwa njia ya mtandao wa kijamii.
Taarifa hizo ni kuhusu kukamatwa kwa mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Zakaria, Peter Zakaria.
Kiongozi huyo ambaye jana alihojiwa na polisi kwa saa kadhaa amesomewa mashtaka na mwendesha mashtaka wa polisi, Kazeni Mrita.
Mbele ya hakimu mkazi Veronica Mugendi, Mrita amedai mshtakiwa amesambaza taarifa hizo mchana wa Julai Mosi, 2018 kwa kuandika kuwa Zakaria alitaka kutekwa na watu wasiojulikana ambao hata hivyo aliwazidi nguvu kwa kuwajeruhi wawili kati yao.
Francis anayetetewa na wakili Onyango Otieno ameachiwa kwa dhamana hadi Jalai 30, 2018 shauri hilo litakapotajwa.
Ametimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja amesaini hati ya dhamana ya Sh2 milioni.