Mwenyekiti wa UVCCM Bukoba vijijini na Bwanku waongoza mazoezi makubwa ya usafi Katerero

Mwenyekiti wa UVCCM Bukoba vijijini na Bwanku waongoza mazoezi makubwa ya usafi Katerero

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
📍Wafanya Usafi Soko la Kemondo.

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Bukoba Vijijini chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Andrew Byera kwa kushirikiana na Afisa Tarafa wa Tarafa ya Katerero Ndugu Bwanku M Bwanku Jumamosi Juni 08, 2024 wameongoza kundi kubwa la wananchi wa Kemondo na Vijana kufanya mazoezi makubwa ya viungo kwa kukimbia zaidi ya Km 10 kwa ajili ya kulinda afya na kujiepusha na magonjwa nyemelezi.

Mazoezi hayo yameanzia kwenye Soko la Kemondo na baadae kufanya usafi kwenye Soko hilo la Kemondo. Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwasasa imekua ikisisitiza sana ufanyaji wa mazoezi kwa wananchi na wito huu wa Serikali unafanyiwa kazi vyema na Umoja wa Vijana Bukoba Vijijini pamoja na Tarafa nzima ya Katerero.

IMG-20240608-WA0040.jpg
IMG-20240608-WA0038.jpg
 
Hongereni sana!, kila nikilisikia hili jina la Katerero, akili yangu inanikumbusha....

Kitabu cha Kiswahili darasa la 4, insha ya "Siku ya Gulioni Katerero"

P
 
Nchi imejaa Mambo ya kipuuzi sana,
Unajiuliza kwa umaskini uliopo kagera, inakuaje swala LA kufanya usafi kwenye soko,na kufanya mazoezi yawe Mambo ya kipaumbele kwa viongozi na wananchi?
Kwanini hatusikii juhudi za kukuza kilimo cha kahawa?
Karne ya 21,dunia inakwenda kwenye mwezi, sie bado tunatangsza jinsi tulivyofanya usafi kwenye soko, jinsi tulivyofanya mazoezi, jinsi tulivyozindua matundu ya vyoo vya zahanati!
Ujmbazi kwenye kahawa, ni wa kutisha, unalima mwenyewe,unapeleka chama cha ushirika, unabwaga pale, haupewi pesa,pesa, itakuja baada ya miezi Sita! Huu ulikuwa, utaratibu miaka ya 90+, sasa hv, kuvuna kahawa taking, mpaka kibari! Ukivuna tu, askari wanavamia wanachukua kisa,taarifa za kiintelijensia zinasema ulitaka kuuza kwa magendo Uganda!
 
Kwa hiyo mtoa taarifa hata namna ya kuweka picha JF hujui?
 
📍Wafanya Usafi Soko la Kemondo.

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Bukoba Vijijini chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Andrew Byera kwa kushirikiana na Afisa Tarafa wa Tarafa ya Katerero Ndugu Bwanku M Bwanku Jumamosi Juni 08, 2024 wameongoza kundi kubwa la wananchi wa Kemondo na Vijana kufanya mazoezi makubwa ya viungo kwa kukimbia zaidi ya Km 10 kwa ajili ya kulinda afya na kujiepusha na magonjwa nyemelezi.

Mazoezi hayo yameanzia kwenye Soko la Kemondo na baadae kufanya usafi kwenye Soko hilo la Kemondo. Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwasasa imekua ikisisitiza sana ufanyaji wa mazoezi kwa wananchi na wito huu wa Serikali unafanyiwa kazi vyema na Umoja wa Vijana Bukoba Vijijini pamoja na Tarafa nzima ya Katerero.
Ukifikaga au ukikaribia uchafuzi hawa watu huwa wanaonesha vipaji vyao vya kuigiza kwa ufanisi mkubwa sana.
 
Hongereni sana!, kila nikilisikia hili jina la Katerero, akili yangu inanikumbusha....

Kitabu cha Kiswahili darasa la 4, insha ya "Siku ya Gulioni Katerero"

P
Umeadimika mzee wetu na mgombea uloyepata kura 0 pale Kigamboni. Vipi 2025 utakuwa tena kwenye kinyang'anyiro au?
 
Back
Top Bottom