GE2025 Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mara, Mary Daniel aibuka Mshindi Kura za Maoni Mgombea Ubunge Serengeti

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mara, Mary Daniel, ameibuka mshindi wa kura za maoni za CCM kuwania ubunge wa Jimbo la Serengeti, akimshinda kwa mbali mbunge aliyemaliza muda wake, Amsabi Amri

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na mratibu wa uchaguzi huo, Abubakar Ghati, Mary Daniel amepata kura 11,533 huku Amsabi akipata kura 1,400, ikiwa ni tofauti kubwa ya kura kati ya aliyekuwa mbunge na kijana anayeongoza umoja wa vijana wa chama hicho

Mbali na wawili hao, Dkt. Kebwe alipata kura 2,903, Michael Mahende kura 1,029, Paul Chacha kura 213 na Deogratias Chacha kura 498. Jumla ya kura zilizopigwa zilifikia 17,981 ambapo kati ya hizo kura 413 ziliharibika na kura halali zilikuwa 17,568

​


Chanzo: Jambo TV
 
Hongera sana Msubhati Mary Michael. Ikawe heri uwe mbunge wa kwanza Mwanamke jimbo la Serengeti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…