Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Baada ya kuwepo kwa concern kutoka kwa wadau mbalimbali kwamba wanafunzi wanatolewa madarasani ili wakaandikishwe kwenye daftari, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mohamed Kawaida amejitokeza kutetea sakata hilo.
Kawaida alisema kuwa ni sahihi kwa wanafunzi kuandikishwa ili wakapige kura iwapo tu watakuwa wamefikisha miaka 18.
Soma pia: Shinyanga: Mwanafunzi wa miaka 16 akutwa na wakala wa CHADEMA akiwa anajiandikisha kwenye Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa. Apigwa maswali mazito!
"Lema analalamika kwa hawa wakurugenzi wanaosajili kwenye daftari la makazi kwamba wanawasajili wanafunzi katika lile daftari. Nikacheka sana nikastaajabu sana na mimi nataka niwaambie watu wa tume ya uchaguzi wasajili wote ikiwa ni wanafunzi au kitu gani. Kikubwa ni kimoja awe ametimiza umri wa kupiga ambao ni miaka 18"
"Anataka kutuaminisha kwamba wale wanafunzi hakuna aliyefikisha umri wa miaka 18. Sasa jamani wanataka tuwapore watu haki zao za msingi? Tunakataa na tunalaani kitendo hiki na tunataka waendelee kuwasajili, muhimu wawe wametimiza umri wa kupiga kura"