Mwenyekiti wa UVCCM Taifa - Siafiki mfumo wa Serikali tatu

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa - Siafiki mfumo wa Serikali tatu

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,482
[h=2]Monday, June 24, 2013[/h][TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]MWENYEKITI UVCCM TAIFA[/TD]
[/TR]
[/TABLE]





[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamisi (katikati) akiwa na mwenyekiti wa UVCCM kilimanjaro, Fredrick Mushi (kulia) na Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Aluu Segamba katika Hafla ya kutunuku Vyeti kwa wanachama wa UVCCM vyuo vikuu Kilimanjaro
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
ARUSHA, Tanzania




MWENYEKITI wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM), Sadifa Juma Hamisi, amepinga vikali kuwepo kwa mfumo wa serikali tatu kama inavyopendekezwa katika rasimu ya katiba.

Sadifa ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wasomi wa UVCCM kutoka katika vyuo vikuu mkoani kilimanjaro katika hafla ya kuwaaga wasomi hao na ambapo pia ametunuku vyeti vya uanachama kwa wanafunzi 312 pamoja na kuwakabidhi kadi za uanachama wanachama wapya.
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="class: tr-caption"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Donge (CCM) zanzibar, amesema uwepo mfumo wa serikali tatu ni mzigo mkubwa kwani kutokana na uduni wa uchumi wan chi yetu itakuwa vigumu kuendesha serikali tatu kwa maana ya serikali ya Zanzibar, serikali ya Tanzania bara na ule wa muungano.

“Jamani tusidanganyane, kuendesha serikali tatu ni mzigo, kwa uduni wa uchumi wetu sidhani kama itakuwa rahisi kuendesha serikali tatu, kama kutakuwa na serikali tatu kuna hatari ya kuvunjika kwa muungano wetu huu maana uwezo kuchangia hatuna, tutajiingiza kwenye matatizo makubwa, vijana tuwe makini na tutumie taaluma zetu kuhimiza umuhimu wa kuwepo kwa muungano huu wa sasa,"


[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="class: tr-caption"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Aidha Sadifa amewahimiza vijana kuwa mfano mzuri kwa jamii huku akiwahimiza kuwa waadilifu, wazalendo, kujiamini na kuwa na nidhamu hali ambayo itasaidia kuwepo kwa amani na usalama wa nchi.


Amesema bila amani na muungano wa wananchi maendeleo hayawezi kupatikana katika nchi ambpo aliwataka vijana kuwa mtari wa mbele kuwaelimisha wananchi wa kawaida juu ya umuhimu wa kuenzi, kudumisha na kuimarisha muungano wa zanzibar na Tanganyika kama njia pekee ya kuhakikisha nchi inakuwa na amani siku zote.


“Vijana tuna wajibu kubwa wa kuwaenzi waliotuletea muungano wetu wa sasa, taaluma zetu ziwe dira ya jamii katika kuenzi, kudumisha na kuimarisha muungano wetu kwani ndio njia pekee ya kusaidia kudumisha amani na usalama wan chi yetu, tuepuke kujiingiza katika mkumbo wa wale wanaodai nchi haitatawalika,” amesema


Hata hivyo Sadifa amewataka vijana kutodanganyika na vyama vinavyoeneza chuki na maandamano yasiyokuwa na msingi wowote huku akifafanua kuwa kisheria kuandamana na haki ya msingi lakini ifuate sheria na yassingilie haki za wengine.


“Chama pekee katika nchi hii ni CCM, kuna vyama vingine vimeanzishwa ambavyo mimi binafsi naviita ‘Saccos’, hauwezi ukajikopesha fedha kienyejienyeji kama alivyofanya Dk. Slaa! Vijana tuwe makini na saccos hizi ambazo ajenda zao ni kukopeshana na vurugu tu,” amesema Sadifa

Kwa upande wake mwenyekiti wa shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu wanachama wa CCM kilimanjaro, Wakati Mtulya akizungumzia changamoto wanazokumbana nazo, alisema kumekuwa na urasimu ndani ya bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, ambapo mikopo imekuwa ikitolewa kwa watu wasiostahili huku walengwa wakiendelea kutaabika.
Amesema kuwa kumekuwa na mchezo ndani ya bodi hiyo, ambapo mikopo imekuwa ikitolewa kwa watoto wa matajiri huku wastahili ‘watoto wa wakulima’ wakibaki kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ya kupata mikopo hiyo jambo ambalo limekuwa likichangia kuwepo kwa vitendo vibaya miongoni mwa wanafunzi hao.


“Mikopo ni yetu, sio ruzuku, lazima tukopeshwe kwa wakati kwani lazima tutairudisha lakini jambo la kusikitisha, bodi hii imekuwa ikitoa mikopo kwa watoto wa masaki, huku sisi watoto wea mkulima tukiendelea kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ili kupata mikopo hiyo, hili ni tatizo,” amesema Mtulya (habari na TAIFA LETU.com).
 
Huyo lazima apinge sii mnzanzibar? anafaidi sana huku bara.watanganyika hatuna faida na muungano
 
Sadifa sema ukweli kizazi cha sasa hakidanganyiki na uongo wa ccm, wasio taka mfumo wa Serekali 3 inamaa hawapingi tu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Bali kibaya zaidi ni kuwanyima haki Watanganyika kuwa na Tanganyika yao na mambo yao yasio ya Muungano. Huwezi kusema Sadifa kuwa Muungano wa sasa ni wa Tanganyika na Zanzibar no. Ni wa Tanzania na Zanzibar, Sasa tukiendelea kuwa na Muungano wa aina hii ni sawa na kuwa na nchi mpya itwaya Tanzania ambayo imeiua Tanganyika na historia yake na mambo yake. kusema Sadifa kuwa mfumo wa serekali tatu ni harama hii sikubaliani na wewe kwa mtazamo wako. Mh Warioba ameona mbali na kapunguza harama zaidi za Serekali , pale alipo Fanya kuwa Bunge kuwa na Wabunge wasio zidi 70 na Mawaziri 15tu,Hapa Mh Warioba aliangalia mbali. Na jengine ni kuhusu haki za Watanganyika zisizo za Muungano, kama vile Waziri wa mambo ya ndani alivyokuwa Vuai Nahoda hii ilikuwa si jambo la Muungano vipi awe Waziri? hapa palitumika Utashi tu wa ukereketwa wa ccm. Yako mambo mengi tu yanayokwenda kinyume na makubaliano ya Mkataba wa Muungano. ccm kupinga serekali 3 nikuona Tanganyika ifikapo na kuwa na Katiba yake na mambo yake yasio ya Muungano ndio kumbuka ccm Zanzibar kwa kupata nafasi za kuchomekwa chomekwa kwa kutumia utashi wa kichama, ndio ukaona ccm/smz wamelivalia njuga hili kuona tonge yao Mh warioba kaitia Mchanga.
 
Nyie viongozi wa ccm hacheni kutuahadaa hapa, chamsingi kura ya maoni ipigwe wananchi wote tutoe maoni yetu kama tunautaka muungano au hatuutaki, na kama kwamba tunautaka muungano kura ipigwe tena tuchague kati ya serikali moja, mbili au tatu.
Msituletee zenu tumeshachoka na hayo mambo ya muungano kulazimishwa kutoka juu
wanachi tupewe nafasi tutoe maoni yetu kwetu tume maalumu, sio nyie kwa kuwa mnakuwa mnasikika kwenye vyombo vya habari kwa sana mnataka kutulisha makamasi yenu.
Hatudanganyiki, viva tume ya maoni ya katiba.

ni mimi from kiembe samaki
 
hahahaha, kuna thread hapo basi ilikuwa aulizwe mfumo wa serikali moja ungelimfaa zaidi kwa mapenzi yake juu ya muungano, kwa nini ang'ang'anie mbili kwa kisingizio cha kulinda muungano wakati serikali moja ndio ingekuwa na uzito zaidi wa hoja zake. Kutamani kufa kuzimia huwezi..
 
hahahaha, kuna thread hapo basi ilikuwa aulizwe mfumo wa serikali moja ungelimfaa zaidi kwa mapenzi yake juu ya muungano, kwa nini ang'ang'anie mbili kwa kisingizio cha kulinda muungano wakati serikali moja ndio ingekuwa na uzito zaidi wa hoja zake. Kutamani kufa kuzimia huwezi..

Serikali moja ndiyo Suluhisho la Muungano siyo serikali tatu, serikali tatu ni Uroho wa madaraka
 
hahahaha, kuna thread hapo basi ilikuwa aulizwe mfumo wa serikali moja ungelimfaa zaidi kwa mapenzi yake juu ya muungano, kwa nini ang'ang'anie mbili kwa kisingizio cha kulinda muungano wakati serikali moja ndio ingekuwa na uzito zaidi wa hoja zake. Kutamani kufa kuzimia huwezi..
Pana msemo usemao 'bendera hufuata upepo', wazee wa CCM wameona serikali tatu ndio MUAROBAINI wa muungano wetu sasa na yeye anakiri hivo moyoni mwake ila nadhani anangoja kauli ya mwenyekiti wake!!!!!!!
 
Serikali moja ndiyo Suluhisho la Muungano siyo serikali tatu, serikali tatu ni Uroho wa madaraka
Mkuu serikali moja haitowezekana sababu ya HISTORIA ndio maana hakuna USSR, Yugoslavia, Czechoslovakia, Ethiopia (kumbuka waliungana na Eritrea) n.k. Ndio maana baba wa taifa ilimshinda hii.
 
Kuna haja ya kuambiwa hii gharama ya serikali tatu ni ipi kwani maneno yamekuwa mengi
 
Back
Top Bottom