Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
📌 📌 Ubungo-NIT Mabibo
🗒️ 29 Agosti 2024
Mwenyekiti wa UWT mkoa Dar es salaam Ndugu Mwajabu Rajabu Mbwambo alikuwa Mgeni Rasmi katika kongamano la Mwanamke Jitambue lililondaliwa na Kablu ya Michezo ya jadi (KLAMIJAMA) iitwayo I Love Mabibo Chini ya Makamu Mwenyekiti Tatu Papa na katibu Mushtaki Khailula Lengo kuu la Kongamano hilo ni
Kutoa elimu ya kukuza uchumi kwa wanawake, utunzaji wa afya, Ushiriki katika Uchaguzi serikali za mitaa na serikali kuu na Elimu masuala ya ukatili wa jinsia na malezi na afya ya akili.
Mwenyekiti Mwajabu aliwaasa wanawake ili kuweza kufikia malengo yao hawana budi kuepukana na vikwazo saba (7) vinavyowazuia wanawake wengi kushindwa kusonga mbele na kuhakikisha wanakabiliana navyo ili kutimiza ndoto zao ambavyo ni;
- Kutokusamehe na kuendeleza magomvi, kujitathimini kusamehe na kusonga mbele.
Pia amehamsisha wanawake kushiriki uchaguzi serikali za mitaa kwa kujiandikisha daftari la mkaa,i na kujitokeza kugombea nafasi za uwenyeviti serikali za mitaa.
Soma Pia: Mwenyekiti UWT Dar, Mwajabu: Juhudi zetu wanawake hazipotei bure zimepelekea kuinuana kiuchumi
#uwtimara
#jeshiladktsamiadktmwinyi
#Kaziiendelee
#ushindinilazima
#mitanotena
©️Uchaguzi Serikali za mitaa 2024

- Tabia ya kukata tamaa waiwache na kutimiza malengo na ndoto zao. Hata kama wataanguka mara kadhaa lakini kukta tamaa ni mwiko.
- Kutegemea watu wengine kubadili maisha yao, jukumu hilo lipo mikononi mwao na si vinginevyo.
- Kuto kujiamini, wakati ni sasa kujiamini na kutegeleza ndoto zao.
- Kukosa uimara wa kihisia, kuhakikisha wanadhibiti mihemko ili isiwe ni kikwazo na kushindwa kuendelea, badala yake kupelekea kuingia katika mitego inayopelekea anguko lao.
- Kutokusamehe na kuendeleza magomvi, kujitathimini kusamehe na kusonga mbele.
- Kuambatana na watu wasiofaa kuwa na marafiki sahihi na wenye malengo ya kimaendeleo badala ya marafiki wa kupiga umbea, porojo na kusengenya wengine. Kuwa na marafiki wa kujadili masuala ya kujikwamua ya kiuchumi na kutafuta fursa za kujifunza kuelimika na kuwekeza akiba.
- Kutokuwa na mpango wa mafanikio kifedha Kuweka mipango imara ya kifedha kwa ajili ya kujiendeleza binafsi, biashara au taasisi unayoiongoza. Wakati ni sasa kupunguza kuvaa sana sare za kila shughuli pesa hiyo itumike katika uwekezaji na unaweza kuanza kuwekeza kidogo kidogo.