Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Veronica Vicent kujitafakari juu ya utendakazi wake ndani ya Wilaya hiyo.
Your browser is not able to display this video.
Chatanda amesema kuwa amesikitishwa na namna ya utendaji kazi wa Mkurugenzi huyo ambavyo hauko vizuri kwenye Halmashauri hiyo ikiwemo mahusiano yake na wenzake.
Chatanda amesema hayo leo Septemba 21, 2023 Wilayani Busega alipokuwa akiagana na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega sambamba na watumishi kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi wilaya humo.
"Mwambieni Mkurugenzi asimame vizuri, narudia tena Mwambieni Mkurugenzi asimame vizuri, hayuko vizuri... ashirikiane na wenzake, ashirikiane na Chama ili mambo yaende vizuri.
"Nimesikitishwa sana na tabia ya Mkurugenzi wa hapa Busega amekuwa sio mtu wa kushirikiana na wenzake, hili suala halikubaliki kwani viongozi wa Chama ndio wenye Ilani ya CCM, hivyo basi anapashwa kuwashirikisha kwenye kila suala linalohusu maendeleo kwenye Wilaya hii," amesema.
Hivi ni mm tu sielewi au hata naninyi pia? Yaani huyu mama , akisema DED angolewe na kweli atapisha njia? Hivi majukumu yake na ya ded kuna mahali wanakutana kweli? Au ni nini !!
Wao wanadhani kila mtu anataka siasa..waweke kina mwijaku au babalevo au steve nyerere kwenye hizo nafasi ili watumikie siasa. Ukiwaweka wasomi na watu wenye proffesional zao wao wanatenda kisomi siasa piga chini.