jamesmwakalinga
Member
- Oct 17, 2024
- 6
- 7
Siku chache baada ya kuzagaa kwa taarifa za tukio la kada wa chama cha mapinduzi(CCM),Ibrahim Shayo a.k.a Ibraline kumshushia matusi mazito meya wa manispaa ya moshi,Zuberi Kidumo,wanachma wa chama hicho wamemwijia juu mwenyekiti wao moshi mjini,Faraj Kibaya Swai.
Taarifa kutoka kwa baadhi ya wanaccm moshi mjini zinadai kuwa,mwenyekiti huyo amekuwa akijaribu bila mafanikio kumsafisha kada huyo ambaye mpaka sasa yupo chini ya adhabu baada ya kupewa onyo na chama hicho kutokana na mwenendo wake usioridhisha ndani ya chama.
Mapema mwanzoni mwa mwaka huu Ibraline na makada wenzake kadhaa waliitwa kwenye kamati ya maadili ya chama hicho ambako walisomewa tuhuma zao na baadae kupewa adhabu ya onyo.
Hata hivyo taarifa zinadai kuwa,faraj Swai ambaye ni swahiba wake mkubwa na kada huyo amekua katika harakati za kumpambania asipewe adhabu nyingine baada ya tuhuma zake nyingine kuwasilishwa ofisi za ccm Taifa,mkoa na wilaya zikimtuhumu kujihusisha na vitendo ambavyo vimekatazwa kwa mujibu wa kanuni za uongozi na madili za ccm na jumuiya zake toleo la 2022.
mapema wiki iliyopita mwenyekiti huyo aliitisha kikoa kilichohusisha wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya huku Ibraline akijumuishwa kwenye kikao hicho ambacho yeye si mjumbe.
Inadaiwa kuwa,kikao hicho kiliitishwa na mwenyekiti kwa nia ya kusaka suluhu dhidi ya Ibraline na makada wenzake ambao wamekuwa katika misuguano inayotokana na kada huyo kutoheshimu kanuni za chama.
Mtoa taarifa wetu aliyekuwa sehemu ya kikao hicho amejulisha kuwa kikao hicho kilivurugika na hapo ibraline alipoanzisha zogo na kumporomoshea matusi mazito meya huyo .
Waliohudhulia kikao hicho mkuu wa wilaya ya moshi(DC),mkuu wa usalama wa Taifa wilaya(DSC),mbunge wa jimbo la moshi mjini(cm),priscus Jacob Tarimo,katibuwa ccm wilaya na meya wa manispaa ya moshi(ccm),Zuberi Kidumo,ambao hawa kwa mujibu wa kanuni ni wajumbe isipokuwa Ibraline pekee.
Lengo la kuitishwa kwa kikao hicho ilikuwa ni kuwepo na upatanishi na taarifa ya upatinishi huo ipelekwe ofisi ya chama mkoa ili kada huyo asikumbane na adhabu nyingine ambayo ni kalipio kali adhabu ambayo inaweza kusababisha kupoteza uanachama wake.
"Maana yake ni kwamba mwenyekiti baada ya kikoa angeandaa taarifa na kuipeleka ofisi ya ccm mkoa ili ionekane watu hawa wamekwishapanishwa ili asiongezewe adhabu kulingana na malalamiko ambayo yapo ccm mkoa",amesema mtoa taarifa wetu.
Kada huyo adaiwa kuwa anapata sapoti kutokana na kuwa karibu na viongozi wa ccm ngazi ya Taifa akiwamo Katibu wa NEC Organization,katibu wa NEC SUK na mmoja wa wabunge wa jimbo moja la uchaguzi mkoani Arusha.
KANUNI ZA UONGOZI NA MAADILI ZA CCM NA JUMUIYA ZAKE ZINASEMAJE?
Kanuni za uongozi na maadili za ccm na Jumiya zake toleo la 2022 zimeainisha mambo yasiyoruhusiwa ambayo mwanachama wa ccm anayetarajiwa kugombea nafasi ya uongozi eneo husika haruhusiwi kuyafanya.
Moja ya mambo hayo ni pamoja na utoaji wa michango,misaada au zawadi za vifaa au nyenzo kwa mtu au shughuli yeyote mpaka iwe tu kwa ridhaa ya kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya ngazi inayohusika kwa masharti kwamba kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa inapata taarifa.
Kwa kuzingatia kanuni hiyo sehemu ya 6 {2} {C} kada huyo wa ccm amekuwa akijihusha na utoaji wa michango katika maeneo mbali mbali misaada,zawadi.
Kwa faida ya wasomaji wa ukurasa huu tunaiweka kanuni ya 6{2}{c} kama inavyojieleza
{2} Kwa hvyo mwanachama haruhusiwi kufanya yafuatayo
{c} Kutoa michango,misaada au zawadi za vifaa au nyenzo kwa mtu au shughuli yeyote mpaka iwe tu kwa ridhaa kamati ya siasa ya Halmashauri kuu ya ngazi inayohusika kwa masharti kwamba kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa inapata taarifa.
Kutoa michango,misaada,zawadi nk.katika eneo ambako mwanachama huyo anakusudia kugombea nafasi yeyote ya uongozi na endapo katika mazingira maalumu ruhusa imetolewa kama ilivyofafanuliwa katika vifungu 6{2}{a} na 6{2]{b}basi mchango huo hautatangazwa.
mwisho.