Kwasababu sipendi kuulizwa/uliza "unatoka wapi" napenda tuagane. Hata kama hayupo nyumbani na unatoka kwa zaidi ya saa moja unaweza ukamtext tu kwamba "natoka kidogo, ntakurudi nyumbani baada ya muda fulani". Hivyo hata akifika akakukosa hatokua na maswali ya wapi ulipo, wakati gani uliondoka na wakati gabi utarudi. Na swala la kusubiria eti mpaka mmoja ajipare au avae ndio aseme 'natoka' sio zuri sana. Ni vizuri mkaambiana mapema ,let say kabla ya kuingia bafuni ili kama mwenzako nae alikua na mipango mingine hata kama haikuhusishi (huhitajiki kujumuika nae) ujue na yeye ajue yako kisha mkubaliane kama kuna cha kukubaliana.
Hata "naenda dukani mara moja", "namuona fulani hapo nje" ni muhimu, you never know what might happen. Unaweza ukakabwa kabari nje au hata ukaanguka mwenzio asijue na wala asiwe na wasiwasi maana anajua utakua jikoni tu au uko humo humo ndani unahangaika na mambo yako.