Naungana na mdau hapo juu kuhusu muda wa Biashara kufikia miaka miwili na kuona inashuka.Hapo kuna tatizo
Kwanza Lazima tukujue Tabia yako.
Maana hata mlevi ukimkuta Bar atakuambia hajalewa ila yeye amepita tu hapo kajikuta anayumba.
Biashara nyingi hizi huwa zinachangamoto nyingi
-Kwanza ni kiashiria kizuuuri sana cha madem,ukihonga hata lips stick basi jua umejimaliza mwenywe
-Lugha,mara nyingi wenye mali,huona kwamba wao ndio kila kitu hasa siku za mwanzo wa biashara,sasa inawezekana kwamba uliharibi tangu mwanzo na umeshindwa ku pick tena.
-Kuna uptodate,kwenye matoleo ya bidhaa,sasa sijui kama unaenda na wakati huo.
Sasa kama kuna moja kati ya hayo,fanya madiliko,moja ikiwemo tafuta mtu umuajiri kwa miezi sita uone nini kitatokea.
sio kila mwenye biashara anaweza kuwa muuzaji mzuri.Ku deal na kinadada inataka moyo saana,na ukikera tu basi wanatabia ya kususa kwa muda mrefu,na wakiambizana ndio kifo chako cha biashara.
We angalie wale chinga wanaopaka madada rangi za kucha,yaani akienda kwenye kijiwe basi wanaambizana huyu jamaa yupo vizuri basi anaunganisha kazi hapo hapo.
La ziada tathmini Location yako.