Mwenzenu lipo linalonisibu naombeni msaada...

condorezaraisi

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2011
Posts
225
Reaction score
116
Poleni sana na huu msiba mkubwa uliotupa wana JF

Naomba msaada wenu kimawazo, Nimeolewa na nina watoto wawili...Mtoto wangu wa kwanza wa kiume nilimzaa nikiwa form two ,nikamrudisha home kwa bibi yake akipata matunzo na mie kuendelea na masomo mpaka hapa nilipofikia katika umri na kazi yangu hii,
Tangu nimezaa mtoto yule sikuwahi kupata matumizi yoyote toka kwa baba yake ingawa kwetu alipafahamu vyema..nimemtunza kwa taabu sana huku nikisaidiwa na wazazi wangu.

Mpaka pale nilipopata kazi na mme ambaye alichukua majukumu ya kumtunza mtoto kama wake.
Leo hii mtoto wangu kamaliza darasa la saba. Mara nikaanza kupokea msg nikiulizwa mtoto wangu kafaulu mwez Dec sikujibu ? nikajua tu huyu sasa atakuwa baba wa mtoto kaanza kujileta..zileendelea kuingia msg mfululizo ambazo nilikaa kimya .

Baada ya kuona imekuwa kero na hizo msg ndipo nikaona nimpigie simu na kumwambia ndio mtoto amefaulu na baba yake anamtafutia shule nzuri ili ampeleke, Yakaanza kuporomoshwa matusi

Ooh mtoto wangu ushamu- adopt nakumpa baba mwingine ,Naona wewe mwanamke ni mpumbavu sana unajifanya una ndoa eeh ,kuna baba mwingine zaidi yake ,umeona nimeshindwa kumsomesha mtoto wangu,tena naanza taratibu za kumfata mwanangu na nitatafuta namba ya huyo mmeo nimwambie akae akijua huyu sie mwanaye ni mwanangu mie

Nilibaki nimepigwa butwaa huku nimeshikilia simu na kukosa la kumjibu ...kwani sikutegemea maneno kama hayo at that time
Baada ya hapo akaendelea kutuma msg za kashifa sikujibu msg hata moja ila nimebakia nawaza sina hata jibu mie mtoto alishaenda shule.

Jamani nimfanyeje huyu mtu wa kuanza kunitukana bila kosa..

NB: Namba zangu alizipata pale alipopiga simu kazini kwetu nikiwa nimesafiri sijui alisema nini mpaka akapewa namba zangu,
 
cha kwanza kufanya mpe taarifa mmeo!then jadilianeni nini cha kufanya!!ukikaa kimya na sms hizo ikatokeo mwenzio kaziona unaweza ukawa na mgogoro wa pili kuutatua!
 
Watu bwana! Mpe za uso tu, muambie kwanza huyo mtoto hakuwa wake ulimchakachulia. Mpige mkwala memchukulia RB na usiwasiliane nae tena. Ni muhimu kushauriana na mumeo ukizingatia amekuwa baba wakati wote muhimu kwa mwanao.
 
siku zote alikua wapi,sas hivi ndo anajua kwamba ana mtoto...ovyooo..we cha msingi mpotezee na akiendelea nenda kamshtaki,arudishe gharama zote ulizotumia kumlea na kumsomesha huyo mtoto mpaka alikofikia..uone kama taendelea tena!!!
 
eeh Pole sana huyo mwanaume kaona mtoto amekuwa sasa ndio anajitokeza ? dunia haiishi vituko pole sana nadhani ni vyema ukamshirikisha mmeo katika hili isije kuzua balaa tena mbeleni
 
Nenda karipoti police na full infomation na ustawi wa jamii kwa msaada na utatuzi zaidi
 
isikuumize kichwa huyo mjingamjinga, mweleze mmeo then mpigie kimya akiendelea kukufuatafuata mchukulie hatua za kisheria.
 


ASEE pole sana dada angu, kwakweli hapa mlipofikia nipagum sana. chamsingi kaa chini na huyo mumeo ambaye ukonae kwa sasa mweleze hari harisi kuhusu huyo mzazi mwenzio, yaani mweleze kiunagauba usimfichechochote. Mweleze kuhusu sms na ambavyo alivyokujibu baada ya kumpigia simu afu usikie yeye atasema nini. Pia usisahau kumuomba mungu maana kupitia yeye kilajambo linawezekana, usiwaze sana piga moyo konde jipe moyo ili uweze kumshinda huyo shetani ambaye anataka kukuharibia amani na furaha katika ndoa yako.
 
Pole mwaya ila jambo la kwanza mshirikishe mumeo tena haraka kabla hajapata taarifa kutoka kwa mtu mwingine.
 
pole sana bi dada

mijanaume mingine hovyoooo kabisa, tena liharuibifu hilo

mueleze mumeo, na hilo janaume likukupigia mwambie huyo mtoto sio wake ebbo

message usizifute ni ushahidi huo, na kama mdau mmoja hapo juu alivyosema toa taarifa polisi kwa matusi uliyopewa na kacheki ustawi wa jamii wanasemaje

hizo ni changamoto, tu huyo mwanaume ni looser tu hana dili
 
Wewe lazima usifiwe, mana umeanza kuzaa kabla ya kufunga ndoa...Usipige kelele mana kuzaa nje ya ndoa hizo ndo zawadi zake.
 
Kaa ukijua, shetani akianguka hutafuta wa kuanguka naye.
Kakaa, kaona mai9sha yako yanaenda vizuri, una amani, una mme, sasa anataka akutie karaha zisizo na tija

Mwambie mmeo mapema, ili aone na yeye ni part ya kutafuta suluhisho.
Msaada wa kisheria unahitajika zaidi.
 
Pole shosti, huyu mwanaume asikunyime raha keshapigwa na chini huko anakotoka ndio anatafuta njia yakukuingia pole pole,mweleze mumeo tena kama ningekua mie hata jina la baba wa mtoto ningeshalibadili kitambo sana sababu wajinga kama hawa ndio wanaovunja ndoa za watu.
 
Hii inaonesha ukomavu wako. Asante kwa kutusaidia kukuelewa ni wa aina gani.

Wewe lazima usifiwe, mana umeanza kuzaa kabla ya kufunga ndoa...Usipige kelele mana kuzaa nje ya ndoa hizo ndo zawadi zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…