Mwenzenu lipo linalonisibu naombeni msaada...

Watu wengine badala ya kushauri wanahukumu,nyie ni wasafi sana enhe.Kosa husamehewa, kosa ni kurudia kosa.Dada C,mshirikishe mumeo,na kama baba wa mtoto yuko tayari kumsomesha mwanae,mumruhusu,mtoto ana haki ya kumjua na kuhudumiwa na baba yake.
 
Dada badilisha hiyo namba ya simu huyo mwanaume ni mjinga achana naye kama alikuwa anajua huyo ni mwanae mbona hajajitokeza hapo mwanzo
 


Pole Condoreza hayo ni mapito ya maisha huna haja ya kujichukia songa mbele ushaweza na utaweza ..mtumaini mungu
 
liwe fundisho kwa wanawake wote kuwa ukishazaa na mwanaume ukae ukijua ata apote baadae either baba au mtoto mwenye atataka kumjua mtoto au baba yake...hivyo mkiwa mwanasa mimba mlijuwage hilo sio mwajiachia tuu

Hilo tunalijua sana na ndo maana hatutaki shari. Unikimbie 13yrs nihangaike na mwanangu nimlee kwa tabu alafu baada ya kukua ndo unakuja na ubabe na matusi juu?? Unacheza wewe...!!! Njoo kwa ustaarabu tutaongea kiustaarabu lakini ukijifanya mjuaji wa kuniletea ukorofi mie imekula kwako, nitakwambia subiri mwanao akikua atakutafuta mwenyewe......UPOO!!!
 
Iman yangu ya dini inaweka bayana kuwa mtoto aliyezaliwa nje ya NDOA,ni wa mama,so mtoa mada huyo ni mwanao tu
 
Watu wengine badala ya kushauri wanahukumu,nyie ni wasafi sana enhe.Kosa husamehewa, kosa ni kurudia kosa.Dada C,mshirikishe mumeo,na kama baba wa mtoto yuko tayari kumsomesha mwanae,mumruhusu,mtoto ana haki ya kumjua na kuhudumiwa na baba yake.

Umeongea vema kabisa ndugu yangu, ila wanawake hatuachii watoto kizembe hivyo! Neno haki ya kumjua na kuhudumiwa na baba yake, lina mantiki sana na ni rahisi kulitamka, ila unauhakika kama mwanao atapata huduma stahiki?? Hakatazwi kuhudumia hata akiwa kwake, mambo ya kumpeleka mtoto alafu anafika anageuzwa houseboy nani anapenda?? Alikuwa wapi kukesha wakati ngoma imenoga, sasa hivi kumepambazuka na watu wanaingia kazini ye ndo anakumbuka kibwebwe?? Hana hata haya.....najua na mengine yamo humu humu!!!
 
Hii inaonesha ukomavu wako. Asante kwa kutusaidia kukuelewa ni wa aina gani.
Wewe unielewe mimi!!!!!

Naona kama unaota vile, endelea kuota si unajua ndoto siku zote ni za bure.
 
asante fazaa kama makosa nilishafanya na wazazi wangu walinisamehe na kunipokea na bado wakaendelea kunipa elimu,hapa nilihitaji ushauri zaidi ,anyway nashukuru kwa mtizamo wako pia
Wazazi kama walikusamehe sawa na mtoto wako ana kosa gani asimjue baba yake.

Yani wewe unaona raha mtoto wako aite mtu mwingine baba, badala ya baba yake khalisi.

Matatizo yako wewe na huyo baba wa mtoto wako, mlipo kuwa mnakata mauno huko nje ya ndoa hamkufikiria kutakuja na mambo kama hayo.....mmemtia jina baya mtoto wenu eti mmezaa nje ya ndoa, ondoa chuki kuwa binadamu, chuki ndo inafanya uzidi kuwa mjinga...wacha mtoto wako amjue baba yake wa damu.
 

Imani yangu, yako, haina uhusiano na haya yaliomo humu. Huyu kazini, kazaa, sasa anakuja na kusema "Jamani nimfanyeje huyu mtu wa kuanza kunitukana bila kosa".

Dhambi zake yeye na huyo aliyezaa nae halafu aje kutuuliza sisi amfanyeje? huu kama si upuuzi ni nini mnaoendelea kuubembeleza?
 

FF, mhusika amekubali ya kuwa amekosa, sidhani kama huu ni muda wa kumponda mwenzetu ambaye yupo njia panda, kwani maji yalishamwagika!!! Shida yake ni ushauri tu ambao utaweza kumsaidia kwa sasa.

Amekubali nini wakati mstari mmoja kabla ya mwisha anasema yeye hana kosa.

Hakuna cha njia panda hapo, anakijuwa anachokifanya asitutie na sisi kwenye upuuzi wake. Sasa anataka sisi ndio tumwambie yeye amfanye nini huyo mzinifu mwenzake? sijui nyie mnasoma hizi nyuzi au mnakurupuka tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…