Kunahitajika elimu ya kutosha kuhusu uwekezaji katika hisa. Unaponunua hisa ujue kabisa kuwa kampuni ikipata hasara na wewe umepata hasara na inapopatkana faida na wewe unapata faida kwa sababu na wewe ni mmiliki wa kampuni hiyo kwa asilimia japo chache. Kwa upande wa NMB sijajua, lakini kila mwaka lazima kunafanyika hesabu na kuona msimamo wa faida na hasara, bila kusahau vikao vya wanahisa kusomewa na kujadili mapato ya mwaka, ikiwemo gawio la faida au hasara(kama ipo), wewe umenunua hisa mwaka gani? na kama haujawahi kualikwa kwenye mkutano wa wenye hisa, na hauna doc yeyote kuonesha kuwa unamiliki hisa NMB hiyo inatia mashaka!!!!!!!!! Hata hivyo suala kama hilo sidhani kama kulileta hapa JF kabla haujaenda NMB kwenyewe kujua kulikoni, nadhani hii pia inatia mashaka kuhusu usiriazi wako katika kuwekeza na kuheshimu pesa yako!! (sorry for that sir!). Pia ikumbukwe kuwa, hisa zako unaweza kuzipiga bei muda wowote unaotaka (kama bei itakuwa imepanda unaweza kupata kafaida kidogo)
Mimi nina hisa chache TWIGA CEMENT, na TCC na kila muda nakwa updated kuhusu mwenendo wa soko.