Mwenzetu anatafuta mwenza/mchumba

Mwenzetu anatafuta mwenza/mchumba

joellincoln

Senior Member
Joined
Mar 20, 2009
Posts
163
Reaction score
19
Katika pita pita yangu kwenye mitandao nimekutana na hii,nafikiri inaweza ikapata msaada zaidi kwa wale wana JF ambao nao wanatafuta wenza. Naomba niquote:

"Mimi naitwa Raymond. Ni mtanzania na elimu yangu ni Masters ya Uchumi kwa sasa niko kikazi Paris, Ufaransa ila nategemea kurudi mwezi ujao. Mi ni mkazi wa Dar es salaam. Natafuta mchumba msichana mzuri anayejiheshimu kabila sichagui na umri uwe kati ya miaka 22 - 30. Mimi nina umri wa miaka 31. Sibagui vilevile dini japo ningependa zaidi awe mkristo na elimu yake iwe form six au chuo. Ni vyema kuambatanisha picha kwa yule atayekuwa tayari na email zote zenye picha zitajibiwa haraka ikiwa ni pamoja na kupewa mawasiliano ya namba ya simu.Tunaweza kuwasiliana kwa email: masungamasunga@yahoo.ie"

Haya kazi kwenu dada zetu mlio kwenye search pia.
 
Joellincoln naomba kuuliza....! Hivi mtu huyo jamaa yetu unaweza niambia ni kitu gani hasa kimemfanya hata kutangaza namna hii? Maana me sipaiti picha maana huku home (TZ) warembo wako wengi ni Domo lako tu! Vitu vingine bwana Uzungu mwiiiingi!
 
Mi mwenywe nimekutana nayo nikabaki mdomo wazi mkuu stanluva ila nikasema acha nirushe kwenye jukwaa letu labda atapata msaada zaidi. Nafikiri labda ni uwoga au anataka achague sana. Ila naona kama anataka kurahisisha kazi kwa kupata wale ambao nao wako search kama yeye
 
Na wewe ulikuwa unatafuta nini huko kwenye hiyo site?
 
mkuu nkamangi kwani kuna tatizo kusaidia watu kama hawa? hhahhaha maana swali lako linaweza likawa ni rahisi sana au likawa ni gumu sana kulijibu
 
Joellincoln naomba kuuliza....! Hivi mtu huyo jamaa yetu unaweza niambia ni kitu gani hasa kimemfanya hata kutangaza namna hii? Maana me sipaiti picha maana huku home (TZ) warembo wako wengi ni Domo lako tu! Vitu vingine bwana Uzungu mwiiiingi!

Kutafuta mchumba mtandaoni nako ni uzungu? Ama kweli ukistaajabu ya Mussa utaona ya firauni
 
huyo mchumba alikwepo sasa hivi sijui kaelekea wapi
we mchumbaaa! we mchumbaeee, he! sijui huyo mchumba
ana matatizo gani? kila akitafutwa huwa haonekani

usijari baba akija tumwambia
 
Back
Top Bottom