Mdau - thanks for thinking. Hata mimi huwa nawaza mawazo haya mazito. Over the years nimegundua kwamba tabia hii imenifanya niwe mdadisi zaidi hata katika mambo ya kawaida na niko informed sana. Kiufupi ni kwamba hakuna bomu la Nyukia lenye nguvu kwa sasa linaloweza kuleta madhara makubwa kwa mwezi. Kwa sasa ukipiga kibomu chako cha Nyuklia, inawezekana huku duniani wala tusijue what is going on. Kimbembe ni pale ikitokea another big heavenly body igongane na mwezi na kufanikiwa kuumega mega au kuusambaratisha kabisa.
Kama heavenly body kubwa ikifanikiwa kuusambaratisha mwezi kabisa, miamba michache ya mwezi inaweza kupenya na kutudondokea hapa duniani. Hatari zaidi hata hivyo itatokana na kutokuwepo kwa mwezi wenyewe. Bila mwezi maisha yetu hapa duniani yatakoma. Mwezi unai-stabilize dunia na kuifanya ibakie katika njia yake bila kutetereka. Hili ni jambo la muhimu sana katika maisha yetu hapa duniani kwani dunia ikisogea kidogo tu mbele au nyuma basi jua linaweza kutuletea matatizo ama kwa joto hapa duniani kuwa kali sana au tunaweza ku-freeze permanently. Yote haya yanaweza ku-disrupt Photosynthesis, na bila Photosynthesis inamaanisha hakuna chakula na hivyo kifo kwa wengi wetu.
Bila mwezi wa kui-stabilize dunia yetu pia dunia inaweza kuongeza au kupunguza spidi yake. Wanasayansi pia wanasema kwamba without the moon, the Earth will start to wobble on its own axis utadhani mlevi wa viroba. Yote haya mawili siyo mambo mema kwani yanaweza kuingilia mfumo wa majira na kuufanya mfumo mzima uparaganyike. Jambo la hatari hata hivyo ni kwamba mambo haya yanaweza kusababisha Magnetic Field ya dunia kufifia sana na kuacha atmosphere yetu ikiwa wazi tu. Kumbuka kuwa Magnetic Field ya dunia ndiyo inatulinda na radiation na kufanya dunia yetu iwe na atmosphere. Bila magnetic field yenye nguvu radiation kutoka kwenye jua (hasa wakati wake wa plasma eruption) itaweza kudhuru viumbe hapa duniani (mbali na kukaanga grid zetu za umeme permanently). Kibaya zaidi ni kwamba bila ulinzi wa kutosha tunaopewa na magnetic field ya dunia, radiation kutoka kwenye jua inaweza kutafuna atmosphere yetu kabisa. Na hili likitokea then it is the end of the game. That means there is no Hydrological Cycle na hewa kama tulivyozoea. Life as we know it will end on this planet!
Japo tunaudharau na tunaukumbuka tu pale unapotumulikia usiku, kufanya bahari zetu kupwa na kujaa na kutufanya tule pilau wakati wa Eid, mwezi una umuhimu mkubwa sana katika mfumo mzima unaoifanya dunia yetu kuwa makazi ya mabilioni ya viumbe hai tukiwemo sisi wenyewe. We owe our very existence to the moon!